• Russia: Marekani inahatarisha umoja wa ardhi yote ya Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov amesema Marekani inachukua hatua hatarishi na za upande mmoja ndani ya ardhi ya Syria zinazohatarisha umoja wa ardhi yote ya nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari akiwa na waziri mwenzake wa Ubelgiji Didier Reynders na kubainisha kuwa: Marekani inafanya kila njia ili kwa kuchukua hatua hatarishi za upande mmoja iweze kufanikisha mkakati wa kuundwa "aina ya nchi" katika eneo kubwa la ardhi ya Syria katika ufukwe wa mashariki wa Mto Euphrate na karibu na mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Iraq.

Lavrov ameongeza kuwa kwa mtazamo wa Moscow, inavyoonyesha, Marekani inatafuta njia ya kuweza kupiga kambi kwa muda mrefu au pengine kusalia moja kwa moja ndani ya ardhi ya Syria.

Vifaru na magari ya deraya ya jeshi vamizi la Marekani ndani ya ardhi ya Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema, ana matumaini Umoja wa Mataifa utahakikisha kunakuwepo na uwazi katika mchakato wa uundaji katiba mpya nchini Syria na kuelekeza juhudi zake katika kukabiliana na wadau wote wa kigeni walioko nchini humo ambao wanaweza kutatiza utekelezaji wa azimio nambari 2254 la umoja huo.

Sergei Lavrov amesisitiza kuwa Russia ingali inaunga mkono kushirikishwa Wakurdi katika mchakato mzima wa amani ya Syria na kwamba bila ya kuwashirikishwa na wao mgogoro wa nchi hiyo hautoweza kutatuliwa.

Marekani, ambayo inajulikana kuwa ni mmoja wa waungaji mkono wakuu wa makundi ya kigaidi nchini Syria, hivi sasa inaendelea kuwepo kimabavu katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.

Mgogoro wa Syria ulianza mwaka 2011 kwa mashambulio makali na ya kila upande ya makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wao kwa lengo kubadilisha mlingano wa nguvu katika eneo la Mashariki ya Kati kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.../

Tags

Feb 13, 2018 16:44 UTC
Maoni