• Mkutano wa Usalama wa Munich; mtazamo hasi kuhusu amani na usalama wa dunia

Mkutano wa 54 wa Usalama wa Munich ulimalizika jana Februari 18 kwa mtazamo hasi kuhusu amani ya dunia.

Mkutano huo ni kongamano la kukutanisha pamoja fikra na mitazamo mbalimbali kuhusu amani na usalama wa kimataifa. Vyombo vya habari vya Ujerumani vimeripoti kuwa, mkutano ambao ulitazamiwa kutoa kipaumbele na kuzingatia suala la amani duniani wenyewe umetoa taswira nyeusi ya hali ya machafuko duniani. Wolfgang Ischinger Mwenyekiti wa Mkutano wa Usalama wa Munich ameeleza masikitiko yake na kuvunjwa moyo na matokeo ya mkutano huo na kusema kuwa: Sisi tumesikia mengi kuhusu hatua zisizo sahihi zilizopo duniani; lakini hatujasikia vya kutosha kuhusu hatua zinazoeleweka ambazo zinaweza kuboresha fikra na mitazamo hiyo hasi. 

Wolfgang Ischinger, Mkuu wa Mkutano wa Usalama wa Munich (MSC)
 

Mamia ya wataalamu na viongozi wa nchi  za mabara matano duniani wameshiriki kwenye kikao hicho cha siku tatu cha Munich Ujerumani.

Washiriki wa Mkutano wa Usalama wa Munich Ujerumani kutoka mabara matano duniani
 

Mkutano wa Usalama wa Munich ni moja ya vikao muhimu kimataifa vya kujadili suala la amani duniani vinavyopewa umuhimu maalumu na duru za kisiasa na vyombo vya habari duniani. Katika mkutano huo wa Munich, viongozi na wataalamu watajika kutoka mabara matano duniani wamajeribu kuwasilisha  mipango ya mapendekezo mbalimbali kuhusu suala la usalama na amani duniani. Mkutano wa Munich wa mwaka huu wa 2018 umejadili na kuchunguza maudhui mbalimbali kuanzia hali ya mivutano katika uhusiano wa pande mbili za Bahari ya Atltantic na vilevile hitilafu zilizopo kati ya nchi wanachama wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato) ikiwemo bajeti ya nchi wanachama wa muungano huo hadi mivutano katika uhusiano wa Magharibi na Russia na migogoro mingine inayolisibu eneo la Mashariki ya Kati.

Sigmar Gabriel, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amekiri waziwazi kwamba: "Sisi leo hii hatuitambui Marekani na wakati huo huo amekuwa kuwepo ufa mkubwa kati ya Ulaya na Marekani", mwisho wa kunukuu. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ameashiria namnadunia hii lo inavyokabiliwa na hatari na kusisitiza juu ya ulazima wa Ulaya kuwa na nafasi zaidi.

 Wolfang Ischinger Mkuu wa Mkutano wa Usalama wa Munich amemkosoa Trump kwa matamshi yake ambayo ni nadra kushuhudiwa na kueleza kuwa, Trump anafanya kila awezalo ili kuirejeshea Marekani nafasi ya ulinzi wa dunia si kwa kutoa vitisho pekee bali hata kwa kutumia silaha; katika hali ambayo nafasi hiyo imepotea kwa miaka kadhaa sasa. 

Baadhi ya serikali kama Marekani na utawala wa Kizayuni zimeubadilisha mkutano huo kuwa fursa ya kuzusha miganwayiko na kutoa vitisho dhidi ya nchi nyingine ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Matamshi yenye utata ya McMaster Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Rais wa Marekani na ya Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni ya kuidhihirisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni tishio na kutoa madai yasiyo na msingi dhidi  ya taifa hili yameakisiwa pakubwa na duru za habari kimataifa. Madai hayo hata hivyo hayakusalia bila ya jibu kutoka kwa Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Wakati huo huo msimamo tofauti uliodhihirishwa na John Kerry Waziri wa zamani wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani umetathminiwa kuwa aina nyingine ya mgawanyiko katika uongozi wa Marekani. John Kerry amesisitiza kuwa, kuna udharura wa kulindwa makubaliano ya nyuklia na Iran kinyume na msimamo wa serikali ya sasa ya Marekani. 

 Benjamin Netanyahu ametoa hotuba isiyo na msingi na madai ya uwongo  katika siku ya tatu ya Mkutano wa Usalama wa Munich. Katika mkutano huo Netanyahu alionekana akiwa na kipande cha chuma mkononi alichodai kuwa ni sehemu ya ndege isiyo na rubani ya Iran na kwa mara nyingine tena akaitishia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Dakta Muhammad Javad Zarif  alijibu matamshi hayo ya Netanyahu na kuyataja kuwa ni maonyesho ya dhihaka ambayo hayana thamani ya kupewa majibu  na kuwataka hadhirina kujadili masuala yenye umuhimu zaidi. 

Feb 19, 2018 12:36 UTC
Maoni