• Muigizaji wa filamu za ngono wa Marekani ampeleke mahakamani Trump

Muigizaji wa filamu za ngono ambaye anadai kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Donald Trump amemshitaki rais huyo wa Marekani, kwa kile alichokitaja kuwa ukiukaji wa makubaliano.

Stephanie Clifford amefungua kesi dhidi ya Trump, ambapo amemtaka Jaji wa Mahakama ya California kubatilisha mapatano kati yake na Trump akidai kuwa upande wa pili umekiuka makubaliano hayo.

Clifford ameitaka mahakama hiyo ifutilie mbali makubaliano kati yake na Trump anayoyataja kuwa batili, akisisitiza kuwa rais huyo wa Marekani hakuyatia saini.

Katika kesi hiyo, muigizaji huyo wa filamu za ngono wa Marekani amesema alikuwa na mahusiano na Trump mwaka 2006, ambayo yaliendelea vizuri hadi mwaka 2007.

Trump na Karen McDougal

Mwezi uliopita, Michael Cohen, wakili binafsi wa Trump alikiri kumpa mwanamke huyo kifumba mdomo cha dola 130,000 za Marekani mwaka 2016, ili asifichue kashfa hiyo ya uhusiano na Trump.

Kadhalika mwezi jana, gazeti la New Yorker la nchini Marekani lilifichua kuwa Trump aliwahi kuwa na uhusiano haramu wa kingono kwa muda wa miezi tisa na mwanamke mmoja mwanamtindo wa jarida la picha za ngono, kwa jina  Karen McDougal.

Tags

Mar 08, 2018 01:41 UTC
Maoni