• Ufaransa yataka kusimamishwa mpango wa makombora wa Iran

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema anachukua hatua kadhaa kwa lengo la kuhakikisha mpango wa makombora ya balisitiki wa Iran unasimamishwa.

Macron ameyasema hayo katika hotuba aliyotoa kwenye kongamano la jumuiya moja ya kizayuni nchini Ufaransa na kukiri kwamba Paris ikishirikiana na waitifaki wake ikiwemo Marekani na Uingereza zinaendelea kuchukua hatua dhidi ya shughuli za makombora ya balistiki ya Iran katika eneo la Mashariki ya Kati.

Huku akiashiria kwamba nchi yake inataka kufanya mazungumzo na pande zote ikiwemo Iran, Rais wa Ufaransa amesema usalama wa Israel si kitu cha kujadiliwa na kufanyiwa mazungumzo.

Kwa mara nyingine tena, Macron amesema rais wa Marekani amekosea kuitangaza Quds kuwa mji mkuu wa Israel na kuongezea kwa kusema: nimemwambia rafiki yangu Donald Trump kwamba amefanya kosa kwa kutoa tangazo la upande mmoja tu kuhusu Quds. Kwa sababu kufanya hivyo hakusaidii kupatikana njia ya utatuzi wa mzozo".

Rais Donald Trump wa Marekani na mandhari ya Quds tukufu

Kwa muda sasa, serikali ya Marekani imekuwa ikizishinikia nchi za Ulaya ziafiki kufanyiwa marekebisho makubaliano ya nyuklia na Iran ya JCPOA na kuanzishwa duru mpya ya mazungumzo na Tehran kuhusiana na maudhui nyinginezo.

Na hii ni katika hali ambayo viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nao wameshatangaza mara kadhaa kwamba hawatofanya mazungumzo yoyote na nchi za Magharibi kuhusu mpango wa taifa hili wa makombora na juu ya masuala ya eneo.../

Tags

Mar 08, 2018 15:59 UTC
Maoni