• Wademokrat watishia kumuuzulu Rais Donald Trump wa Marekani

Chama cha Democratic cha Marekani kimetishia kuwa iwapo Rais Donald Trump wa nchi hiyo atasimamisha uchunguzi wa faili lake la uchaguzi na Russia watamuuzulu kiongozi huyo.

Ripoti zinasema kuwa, viongozi wa chama hicho wametangaza kuwa, iwapo Trump atamfuta kazi Robert Mueller anayeshughulikia faili la uchunguzi kuhusu uwezekano kwamba Russia iliingilia uchaguzi uliopita wa rais wa Marekani, watachukua hatua ya kumuuzulu kiongozi huyo.

Kwa mara nyingine tena Donald Trump amehoji uchunguzi unaofanyika kuhusu madai kwamba Russia iliingilia uchaguzi uliopita wa rais na amepinga muundo wa timu iliyoundwa na Robert Mueller kufuatilia faili hilo. Trump amesema katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa kijamii wa Tweeter kwamba: Ni kwa nini timu hiyo ina wanachama 13 wa chama cha Demokratic na haina Mripublican hata mmoja?

 Lindsey Graham: Kufutwa kazi Mueller utakuwa mwanzo wa kufukuzwa kazi Donald Trump

Viongozi wa chama cha Democratic wanasema kufutwa kazi Robert Mueller ni mstari mwekundu ambao haupaswi kuvukwa. Vilevile wawakilishi wa chama cha Republican katika Baraza la Seneti la Marekani wametahadharisha kuhusu athari mbaya za hatua yoyote itakayochukuliwa na Donald Trump dhidi ya Robert Mueller.  

Seneta Lindsey Graham wa chama cha Republican katika jimbo la South Carolina amesema kuwa, kumfuta kazi Robert Mueller utakuwa mwanzo wa kuondolewa madarakani Donald Trump.    

Mar 19, 2018 15:24 UTC
Maoni