• Rais Putin: Russia haiko katika mashindano ya silaha na nchi za Magharibi

Rais Vladmir Putin wa Russia ametangaza kwamba, nchi yake haiko katika mashindano ya silaha na nchi za Marekani na Magharibi.

Putin ameyasema hayo wakati akiweka wazi mipango yake ya urais wa awamu ya nne nchini Russia na kuongeza kuwa, Moscow haina nia yoyote ya kuingia katika mashindano ya silaha na badala yake ina mpango wa kupunguza gharama za kiulinzi katika mwaka 2018-2019.

Baadhi ya silaha hatari za Russia

Rais Vladmir Putin aliyekuwa amekutana na wagombea wengine waliochuana naye katika uchaguzi wa rais uliopita ameongeza kwa kusema, Moscow imetaka kufanyika mazungumzo chanya na washirika wote wa kimataifa kwa ajili ya kutatua tofauti zilizopo na kwamba pendekezo hilo linapaswa kujibiwa. Kadhalika Rais Vladmir Putin amesema kuwa, kuongeza kiwango cha uchumi nchini Russia ni kipaumbele chake cha kwanza na kwamba, miundombinu ya nchi hiyo itazingatiwa zaidi na serikali ya awamu hii na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi ni suala litakalokuwa na umuhimu mkubwa. Duru ya saba ya uchaguzi wa rais nchini Russia ilifanyika siku ya Jumapili tarehe 18 Machi 2018, ambapo Rais Vladmir Putin alipata ushindi wa mkubwa. 

Silaha hizo za Russia

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume Kuu ya Uchaguzi ya Russia, baada ya kuhesabiwa kura zote, Putin, wa chama cha Russia Iliyoshikamana (Yedinaya Rossiya) amepata asilimia 76.64  ya kura milioni 55.4 na hivyo kuibuka mshindi katika uchaguzi huo.

Tags

Mar 20, 2018 04:25 UTC
Maoni