Apr 19, 2018 07:26 UTC
  • China yaionya Marekani isiingilie masuala yake ya ndani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ameionya Marekani isiingilie masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Hua Chunying ametoa onyo hilo kufuatia matamshi ya afisa mmoja wa serikali ya Marekani aliyedai kuwa makumi ya maelfu ya watu wametiwa nguvuni na askari wa usalama wa China katika eneo la Xinjiang na kusisitiza kwamba haipasi Marekani kuingilia mambo ya ndani ya China.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China aidha ameitaka Marekani iache kueneza habari zisizo sahihi kuhusiana na nchi hiyo.

Rais Xi Jinping wa China (kulia) na Rais Donald Trump wa Marekani

Chunying ameongeza kuwa, watu wa eneo la Xinjiang "wako radhi na hali yao kimaisha na kikazi" na wanafurahia "maisha ya amani na ya maendeleo."

Laura Stone, msaidizi wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Asia ya Mashariki na Bahari ya Pasifiki alidai hapo jana kuwa vikosi vya usalama vya China vimewatia nguvuni makumi ya maelfu ya watu wa eneo la Xinjiang mashariki mwa nchi hiyo.../ 

Maoni