Apr 21, 2018 03:36 UTC
  • Russia: Marekani na washirika wake wanafanya njama nyingi kuigawa Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov amekosoa vikali misimamo ya uhasama ya Marekani ya kutaka ya kuisambaratisha nchi ya Syria.

Lavrov aliyasema hayo jana Ijumaa ya jana katika kikao cha waandishi wa habari mjini Moscow pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria na kusema kuwa, njama kwa ajili ya kuisambaratisha na kuigawa vipande taifa la Syria zinaendelea kupangwa na Marekani. Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, Washington inafanya njama kuzivutia nchi nyingi kwa ajili ya kukamilisha mpango huo. Katika kikao hicho na waandishi wa habari, Sergey Lavrov amezungumzia pia suala la kutumwa askari wa kusimamia amani mashariki mwa Ukraine.

Licha ya njama chafu za adui, lakini wananchi wa Syria wameendelea kushikamana na serikali yao halali

Baada ya kushindwa magenge ya magaidi katika eneo la Ghouta Mashariki nchini Syria sambamba na kufurushwa magaidi hao kutoka eneo hilo, Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi zilizusha madai bandia kwamba serikali ya Damascus imetumia sialaha za kemikali huku serikali ya nchi hiyo ikikadhibisha vikali madai hayo. Cha ajabu ni kuwa, tarehe 14 mwezi huu, Marekani, Uingereza na Ufaransa ziliyashambulia baadhi ya maeneo ya Syria bila ya idhini ya Umoja wa Mataifa na hata kabla ya kufanyika uchunguzi wa kubaini uhakika wa madai hayo, suala ambalo linaendelea kulaaniwa hadi leo hii katika kona mbalimbali za dunia.

Tags

Maoni