Mei 21, 2018 14:12 UTC
  • Marekani yaamua kurudi nyuma katika vita vya biashara ilivyovianzisha dhidi ya China

Waziri wa Fedha wa Marekani ameelezea kusimama vita vya kibiashara kati ya nchi yake na China sambamba na kukubali kupunguza mizozo ya kibiashara baina nchi hizo.

Steven Mnuchin, amesema vita vya kibiashara kati ya Washington na Beijing kwa hivi sasa vimesimamishwa. Matamshi hayo yametolewa baada ya Marekani na China kuafikiana juu ya kuweka mlingano wa kibiashara na kadhalika kuondoa tofauti baina yao.

Steven Mnuchin, Waziri wa Fedha wa Marekani 

Aidha Mnuchin na Larry Kudlow, Mshauri wa ngazi ya juu wa uchumi wa ikulu ya Marekani (White House) wamesisitiza kwamba, wawakilishi wa Marekani na China wamefikia makubaliano Jumatatu ya leo ya kupunguza mizozo ya kibiashara kati ya nchi mbili. Kuhusiana na suala hilo Waziri wa Fedha wa Marekani amesema kuwa, hivi sasa Washington na Beijing ziko katika hali ya kusimamisha vita vya kibiashara na kwamba ushuru wa ziada pia umesitishwa.

Marais wa China na Marekani

Tangu alipoingia madarakani, Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akisuguana na China kwa kuituhumu nchi hiyo ya Asia kuwa ni 'mwizi wa fursa za kazi nchini Marekani' ambapo katika uwanja huo aliweka ushuru mkubwa kwa bidhaa za Marekani. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, nakisi ya kibiashara kati ya Marekani na China ilikaribia Dola bilioni 375 mwaka 2017 pekee.

Tags

Maoni