Mei 22, 2018 14:01 UTC
  • Mwanasiasa wa Russia: Mafanikio ya Iran katika eneo yameikasirisha mno Washington

Mbunge wa ngazi ya juu katika bunge la Russia (Duma) amesema kuwa, siasa za kujitegemea na nafasi chanya na athirifu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo la Mashariki ya Kati, zimeifanya Marekani kupatwa na hasira.

Sergei Vladimirovich Zheleznyak ameyasema hayo akijibu matamshi ya jana ya Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na kuongeza kwamba, orodha ndefu ya matakwa yaliyotolewa na Washington dhidi ya Iran, inaonyesha kwamba kwa mtazamo wa kimataifa Marekani inafuatilia malengo ya kisiasa na kiuchumi tu.

Sergei Vladimirovich Zheleznyak, Mwakilishi wa ngazi ya juu katika bunge la Russia (Duma).

Aidha ameongeza kwamba hatua hiyo ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni uchochezi na vitisho vya wazi. Kadhalika Vladimirovich Zheleznyak sambamba na kuyataja matakwa ya Marekani kuwa yasiyokubalika ameongeza kwamba, katika hali ambayo Washington inadai kuzuia mashindano ya silaha za nyuklia duniani, lakini hatua yake ya kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran (JCPOA) na kwa namna ya wazi kabisa imekiuka mkataba wa kimataifa wa kuzuia kuenea silaha za nyuklia duniani. 

Maadui wa taifa la Iran ambao wanakesha kupanga njama ili kutoa pigo dhidi ya Iran ya Kiislamu

Mbunge huyo wa ngazi ya juu katika bunge la Russia (Duma) ameashiria uingiliaji ulio kinyume cha sheria wa Marekani huko nchini Syria na kadhalika uchochezi wa migogoro wa White House katika eneo la Mashariki ya Kati, mkabala wa nafasi chanya na athirifu ya Iran kwa ajili ya kumaliza mizozo ya eneo na kupambana na ugaidi na kuhoji, ni vipi suala hilo litaacha kuitia fedheha Marekani na Waziri wake wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mike Pompeo? Wakati huo huo, Mwakilishi wa Russia katika Shirika la Kimataifa la Nyuklia amesema kuwa, matakwa ya Marekani dhidi ya Iran ni upuuzi mtupu.

Mikhail Oliyanov

Mikhail Oliyanov amesema kuwa, matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani dhidi ya Iran si ya uwajibikaji kama ambavyo pia sio ya kiakili. Amesisitiza kwamba misimamo hiyo imetolewa bila ufahamu wala weledi wowote. Ameongeza kwamba hatua ya Iran ya kufungamana kikamilifu na mikataba yote kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia, kumeweka wazi ukweli kwamba mkiukaji mkuu wa sheria na mikataba ya kimataifa ni Marekani na wala sio Tehran.

Tags

Maoni