• Russia yawatahadharisha raia wake kuhusu watoto wa nje ya ndoa kombe la dunia

Mkuu wa Masuala ya Familia, Watoto na Wanawake katika Bunge la Russia, Tamara Pletnyova, amesema kamati ya masuala ya wanawake na watoto inawatahadharisha wanawake wa nchi hiyo kuingia katika mahusiano ya kimapenzi kinyume na ndoa katika michuano ya kombe la dunia inayoendelea hivi sasa nchini humo.

Pletnyova ametoa tahadhari hiyo kutokana na taathira mbaya ya mahusiano ya kimapenzi yaliyo haramu ya kuzaliwa watoto wasio na baba hasa baada ya kumalizika kwa michuano hiyo. Kwa ajili hiyo amesisitiza kwa kusema: "Russia inawataka wanawake kutojihusisha kimapenzi na mashabiki ama watu wanaokuja kwa ajili ya fainali hizi kwani inaweza kuwa kama ilivyokuwa kwa michezo ya mwaka 1980 ya Olimpiki ya mjini Moscow, ambapo watoto wengi walizaliwa bila kuwepo wazazi wawili."

Michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Russia kwa sasa

Kadhalika Mkuu wa Masuala ya Familia, Watoto na Wanawake katika Bunge la Russia amewataka raia wa nchi hiyo kufunga ndoa kisheria badala ya kuzini na amesema: “Labda wakubaliane kuoana na inawezekana hawatafanya hivyo, sasa hapo watakaohangaika ni watoto, ambao watapata taabu kama ilivyokuwa kwenye michezo ya Olimpiki ya Moscow.” Kadhalika Tamara Pletnyova amesema: "Ikiwa mambo yatakwenda kama watu wanavyotaka wenyewe, kutakuwa na watoto wengi walio nje ya ndoa." Hata hivyo Bi, Pletnyova amekosolewa na vyombo mbalimbali vya habari duniani kutokana na matamshi yake ya kibaguzi aliyoyatoa kuwahusu watu weusi pale alipowataka wanawake wa nchi hiyo kutofunga ndoa na watu hao na badala yake wafunge ndoa na watu weupe ili kupata watoto wenye asili sawa na ya watu wa Russia.

 

 

 

 

 

Tags

Jun 18, 2018 15:19 UTC
Maoni