Jun 19, 2018 07:36 UTC
  • Russia yatuma manowari zake mbili zilizobeba makombora ya cruise kwenye pwani ya Syria

Jeshi la Russia limetangaza kuwa manowari mbili za jeshi hilo zilizobeba makombora aina ya cruise zimetumwa kuelekea bahari ya Mediterania na pwani ya Syria.

Jeshi la wanamaji la Russia katika kituo cha Bahari Nyeusi limetoa taarifa na kutangaza kuwa: Manowari mbili za Grad Sviyazhsk na Veliky Ustyug zilizobeba makombora ya Cruise zimeng'oa nanga katika bandari ya Sevastopol katika eneo la Crimea.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, manowari hizo mbili zitawasili kwenye bahari ya Mediterania kupitia malango bahari ya Bosporus na Dardanelles na kujiunga na manowari za Russia zilizopiga kambi katika bahari hiyo.

Kombora la manowari ya Grad Sviyazhsk

Manowari hizo kadhaa za jeshi la wanamaji la Russia zimewekwa kwenye eneo hilo la bahari ya Mediterania tangu miaka karibu mitano iliyopita.

Jeshi la Russia limeweka vikosi vyake kwenye maeneo ya maji ya pwani ya Syria na ndani ya ardhi ya nchi hiyo kufuatia wito wa serikali ya Damascus wa kuisaidia katika vita vya kupambana na magaidi.

Russia imeshatumia mara kadhaa makombora yake aina ya cruise yanayolenga umbali wa karibu kilomita mbili kushambulia ngome za kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh nchini Syria.../

Tags

Maoni