Jul 11, 2018 13:41 UTC
  • Kansela Merkel amjibu Trump na kumfahamisha kuwa Ujerumani huchukua maamuzi huru

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amejibu matamshi makali ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya nchi yake na kumfahamisha kuwa, 'Ujerumani inafuata sera na maamuzi huru'.

Mapema leo Jumatano alipokutana na Jens Stoltenberg Katibu Mkuu wa Muungano wa Kijeshi wa NATO, Trump aliiitaja Ujerumani kuwa  ni nchi iliyotekwa na Russia. Trump alidai kuwa Ujerumani inaongozwa kikamilifu na Russia na kwa msingi huo rais wa Marekani amesema si sahihi kwa NATO kuihami na kuilinda Ujerumani. Aidha Trump amelalamika kuwa, Ujeurmani inailipa Russia mabilioni ya dola mkabala wa kupokea nishati. Rais wa Marekani pia medai kuwa Ujerumani ndio inayoifanya Russia iwe nchi tajiri. Mwaka 2016 Ujerumani ilinuanua takribani asilimia 40 ya mfauta yake ya petroli kutoka Russia. 

Rais Trump wa Marekani akiwa na Merkel wakati walipohitiliafiana katika mkutano wa G7 hivi karibuni nchini Canada

Katika kujibu matamshi hayo ya Trump, Merkel amesisitiza kuwa, Ujerumani ndio nchi ya pili muhimu ambayo inachangia wanajeshi katika NATO.

Hivi sasa kumeibuka hitilafu kubwa baina ya wanachama wa muungano wa kijeshi wa NATO na misuguano hiyo imegubika kikao cha muungano huo ambacho kinafanyika leo mjini Brussells Ubelgiji.

Tags

Maoni