Jul 12, 2018 07:29 UTC
  • Wakuu wa Nato wakariri madai dhidi ya Iran katika kikao chao mjini Brussels

Viongozi wa nchi wanachama wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato) wamekariri madai ya Marekani dhidi ya Iran kuhusu miradi ya kiulinzi ya nchi hii. Madai hayo yametolewa kufuatia taarifa iliyotolewa katika siku ya kwanza ya kikao chao hicho mjini Brussels jana.

Nchi wanachama wa Nato jana Jumatano walieleza kuwa wanatiwa wasiwasi na majaribio ya makombora ya Iran na kudai kuwa hatua za kuiulinzi za nchi hii zinasababisha ukosefu wa amani katika Mashariki ya Kati. 

Jaribio la kombora la Emad la Iran

Taarifa ya wakuu hao wa nchi  wanachama wa muungano wa Nato imeitaka Iran kusitisha kile ilichokitaja kuwa ni uungaji mkono wake kwa mhimili wa muqawama dhidi ya utawala bandia wa Israel katika eneo la Mashariki ya Kati.  Katika sehemu nyingine ya msimamo huo wa uingiliaji kupitia taarifa hiyo,  viongozi wa Nato  wameitaka Iran kuachana na miradi yake ya kiulinzi.  

Nchi wanachama wa muungano wa Nato aidha kwa pamoja zimeahidi kuhakikisha kuwa miradi ya nyuklia ya Iran inatekelezwa kwa malengo ya amani, inaendelea kushirikiana na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na kwamba eti haitengenezi silaha za nyuklia. 

Sehemu nyingine ya taarifa ya wakuu wa Nato imesisitiza juuya suala la kuongezwa bajeti ya kijeshi ya nchi wanachama kutokana na mashinikizo ya Marekani. Nato imeendelea kufanya juhudi za kutilia shaka miradi ya nyuklia ya Iran katika hali ambayo kufikia sasa wakala wa IAEA katika ripoti zake nyingi na za mara kwa mara umethibitisha kwamba miradi hiyo inatekelezwa kwa malengo ya amani na Iran kuheshimu ahadi zake zote ilizotoa katika mapatano na nchi 6 muhimu za dunia yanayojulikana kifupi kama JCPOA.

Tags

Maoni