• Mapigano makali kati ya magaidi wa Daesh na Taleban yanaendelea Afghanistan

Mapigano makali kati ya wanachama wa makundi mawili ya kigaidi ya Daesh (ISIS) na Taleban yangali yanaendelea katika mkoa wa Jowzjan, kaskazini mwa Afghanistan.

Jeshi la serikali limetangaza kwamba, mapigano hayo makali kati ya makundi hayo yameibuka katika wilaya ya Darzab na kwamba hadi sasa yangali yanaendelea, huku kundi la Telaban likifanikiwa kudhibiti ngome za wapiganaji wa Daesh. Muhammad Hanif Rezai, mmoja wa makamanda wa jeshi la serikali amesema kuwa mapigano hayo kati ya Daesh na Taleban ni makali na kwamba hadi sasa zaidi ya wanachama 50 wa kundi la Daesh tayari wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa. Ameongeza kuwa, baadhi ya wanachama wa Taleban pia wameuawa na kujeruhiwa katika mapigano hayo.

Marekani muungaji mkono wa genge la Daesh katika vita vya sasa kati ya Taleban na Daesh

Inafaa kuashiria kuwa, katika miezi ya hivi karibuni na kwa mara kadhaa, wanachama wa kundi la Taleban wameshambulia ngome za magaidi wa Daesh. Mji wa Darzab unahesabika kuwa ngome ya magaidi wa Daesh (ISIS) ambao hivi sasa unalengwa na magaidi wa kundi la Taleban. Kabla ya hapo pia Taleban ilishambulia mji huo kwa lengo la kuudhibiti kutoka mikononi mwa Daesh, hata hivyo askari wa Marekani waliingilia kati kwa lengo la kuwasaidia magaidi hao wa Daesh. Hii ni katika hali ambayo, Taleban na baadhi ya viongozi wa serikali ya Afghanistan wamekuwa wakiituhumu Marekani kwa kuwaunga mkono wanachama wa genge la Daesh ambalo limehusika na jinai nyingi za kigaidi katika miezi ya hivi karibuni.

Jul 20, 2018 07:46 UTC
Maoni