Aug 13, 2018 14:44 UTC
  • Iran na Uturuki zahimizwa kuunganisha nguvu zao kupambana na Marekani

Mkuu wa chama cha Vatan cha Uturuki amesema kwamba kuna wajibu kwa Ankara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuunganisha pamoja nguvu zao kupambana na vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi hizo mbili.

Dogu Perinçek amesema hayo leo na kuongeza kuwa, Iran ni mshirika wa kiistratijia na ni jirani mwaminifu kama ambavyo ndiyo nchi inayoidhaminia Uturuki sehemu kubwa ya mahitaji yake ya nishati na ni kwa sababu hiyo ndio maana ushirikiano wa Ankara na Tehran ukawa ni jambo la dharura na muhimu sana katika kukabiliana na ubeberu wa Marekani.

Dogu Perinçek, Mkuu wa chama cha Vatan cha Uturuki

 

Mkuu huyo wa chama cha Vatan cha Uturuki ameongeza kuwa, ushirikiano wa kiistratijia baina ya Tehran na Ankara na ushirikiano mzuri wa nchi hizo mbili katika suala la Syria, bila ya shaka yoyote ni jibu thabiti kwa vitisho vya Marekani.

Vile vile amesema, serikali ya Uturuki inapaswa kuachana mara moja na siasa za kuipiga vita Syria na badala yake ifanye juhudi za kurejea uhusiano na kutoa mkono wa urafiki kwa Damascus kama njia ya kuimarisha ushirikiano uliopo hivi sasa baina ya China, Russia na Iran.

Hivi karibuni Marekani iliziwekea vikwazo vya kidhulma Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki ikiwa ni kuzidi kuwathibitishia walimwengu ubeberu wake.

Maoni