Sep 10, 2018 07:24 UTC
  • Trump kuwafukuza Wapalestina nchini Marekani

Gazeti moja la nchini Marekani limeripoti kuwa, mshauri wa usalama wa taifa wa White House, leo Jumatatu atatangaza kufungwa ofisi ya Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO mjini Washington.

Toleo la mtandaoni la Wall Street Journal limetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, matini ya hotuba ya leo la John R. Bolton, mshauri wa usalama wa taifa wa Donald Trump inaonesha kuwa leo atatangaza kufungwa ofisi ya PLO mjini Washington.

Katika matini ya hotuba hiyo kuna maneno yasemayo: Serikali ya Trump haiwezi kuibakisha wazi ofisi ya PLO mjini Washington wakati Wapalestina wanakataa kuanza mazungumzo ya maana na ya moja kwa moja na Israel.

Trump anawashinikiza kila upande Wapalestina ikiwa ni pamoja na kukata mchango wa Marekani kwa wakimbizi madhlumu wa Kipalestina

 

Gazeti hilo pia limeripoti kuwa, Marekani ina nia ya kuiwekea vikwazo Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kama itaendelea kuchunguza jinai za Wamarekani nchini Afghanistan na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Kabla ya hapo, Donald Trump, rais wa Marekani mwenye fikra za Kizayuni na chuki dhidi ya wageni hasa Waislamu wakiwemo Wapalestina alikuwa ametangaza kukata mchango wa Washington kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Palestina UNRWA na hivi sasa imethibitishwa kuwa hospitali za Palestina hasa za Ukanda wa Ghaza zitafungwa kikamilifu kwa kukosa misaada.

Trump anawashinikiza Wapalestina wakubaliane na mpango wake wa eti "Muamala wa Karne" wenye nia ya kuingamiza kabisa kadhia ya Palestina.

Tags

Maoni