Sep 11, 2018 09:42 UTC
  • Russia yataka kuitishwa kikao cha Baraza la Usalama kujadili mkutano wa pande tatu wa Tehran

Ofisi ya mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa imetoa wito wa kufanyika kikao cha Baraza la Usalama la umoja huo kuchunguza matokeo ya mkutano wa pande tatu wa Tehran kuhusiana na Syria.

Msemaji wa ofisi ya mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa, Fyodor Strzhizhovsky amesema Moscow imetaka kuitishwa kikao cha Baraza la Usalama hii leo Jumanne kujadili matokeo ya mazungmzo ya Tehran kuhusu Syria. 

Itakumbukwa kuwa Ijumaa iliyopita Marais Hassan Rouhani wa Iran, Vladimir Putin wa Russia na Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki walikutana mjini Tehran na kutoa taarifa ya pamoja. Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa mgogoro wa Syria hauwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi na kwamba njia pekee ya kukomesha mgogoro huo ni mwenendo wa kisiasa na kuketi kwenye meza ya mazungumzo. 

Marais wa Iran, Russia na Uturuki

Mada kuu iliyojadiliwa na viongozi hao watatu mjini Tehran ilikuwa hali ya mambo katika mkoa wa Idlib huko kaskazini magharibi mwa Syria na mchakato wa kutatua matatizo ya nchi hiyo.  

Tags

Maoni