Sep 12, 2018 14:15 UTC
  • Michael Moore afichua kashfa ya kingono kati ya Trump na binti yake Ivanka Trump

Mtengeneza filamu maarufu wa nchini Marekani, Michael Moore, amefichua kwamba Ivanka Trump, binti wa Rais Donald Trump wa nchi hiyo ni muhanga wa udhalilishaji wa kingono kutoka kwa baba yake, wakati binti huyo alipokuwa mdogo.

Moore amefichua kashfa hiyo katika filamu yake mpya ambayo imezungumzia sehemu ya maisha ya Rais Donald Trump wa Marekani ambapo imeelezea mienendo mibaya ya kiakhlaqi ya rais huyo dhidi ya binti yake Ivanka. Michael Moore amesisitiza kwamba, Ivanka Trump ni muhanga wa udhalilishaji wa kingono kutoka kwa baba yake. Kadhalika mtengeneza filamu huyo mashuhuri wa Marekani ameonyesha vitendo visivyo vya kiakhlaqi vya Trump kwa kutumia picha zenye kutia shaka kati yake na binti huyo. Kwa mujibu wa Moore, picha hizo za pamoja kati ya Trump na Ivanka zinaonyesha wazi uwepo wa vitendo viovu vya kingono vya rais huyo dhidi ya binti huyo wakati akiwa mdogo.

Rais Donald Trump wa Marekani anayetajwa kuwa mfuska mkubwa

Amesema kuwa, hatarajii majibu ya Trump kuhusiana na filamu yake hiyo mpya juu ya uhusiano wa kifuska kati yake na Ivanka, kwa kuwa mienendo ya Trump inaonyesha wazi kwamba ni mtu muovu na mshari mkubwa. Mbali na hayo ni kwamba, katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2016, Rais Donald Trump pia alinukuliwa akitoa maneno yasiyo ya kiakhlaqi kumuhusu binti yake Ivanka. Ripoti mbalimbali zilizotolewa na vyombo vya habari nchini Marekani, vinamuhusisha Trump na kashfa mbalimbali za kingono. Katika uwanja huo, wanawake kadhaa wameshawasilisha mashitaka ya udhalilishaji huo wa kingono wa Trump dhidi yao.

Maoni