• Imran Khan kupiga mnada leo magari ya kifahari ya ofisi ya waziri mkuu, Pakistan

Magari ya kifahari ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Pakistan yanapigwa mnada hii leo kwa lengo la kutafuta fedha kwa maslahi ya umma.

Ripoti zinaeleza kuwa miongoni mwa magari yanayopigwa mnada ni magari 102 kati ya magari 200 ya kifahari ya Ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo.  Chama cha Tehreek-e-Insaf kinachoongozwa na waziri mkuu huyo kimetangaza kwamba, fedha zote zitakazopatikana katika mnada huo wa magari zitatumiwa katika maslahi makuu ya umma nchini.

Imran Khan, Waziri Mkuu Mpya wa Pakistan ambaye ameamua kuishi maisha ya kawaida yasiyo ya kifahari

Katika hatua nyingine, ni kwamba hivi karibuni Ofisi ya Waziri Mkuu wa Pakistan inatarajiwa kubadilishwa kuwa Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Intelejensia. Kuishi maisha ya kawaida ni moja ya nara muhimu za serikali ya Imran Khan. Inaelezwa kwamba hatua ya viongozi wa zamani wa Pakistan ya kuishi maisha ya kifahari kwa muda mrefu imeibua pengo kubwa la kimatabaka katika jamii ya nchi hiyo. 

Sep 17, 2018 07:53 UTC
Maoni