Sep 18, 2018 14:09 UTC
  • Russia yaionya Israel kufuatia kutunguliwa ndege yake katika anga ya Syria

Kufuatia ajali ya kutunguliwa ndege ya Russia katika anga ya Syria wakati wa shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya nchi hiyo, Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa inayo haki ya kujibu mapigo kwa Israel kutokana na tukio hilo.

Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergueï Choïgou ametoa onyo kwa Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni Avigdor Lieberman na kumweleza kwamba Moscow inaibebesha Tel Aviv dhima kamili ya vifo vya wanajeshi wake 15.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza leo kuwa ndege moja ya kijeshi aina ya Ilyushin 20 (IL20) ikiwa na watu 15 ndani yake ilipotea kwenye rada karibu na kituo cha anga cha Hamimim mkoani Lattakia kaskazini magharibi mwa Syria.

Ndege ya kivita ya Russia aina ya Ilyushin 20 (IL20)

Mbali na kubainisha kuwa ndege yake hiyo iliyotoweka wakati wa mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Lattakia ilitunguliwa na vikosi vya ulinzi wa anga vya Syria, Wizara ya Ulinzi ya Russia imesisitiza kuwa marubani wa Kizayuni waliitumia ndege hiyo ya Russia kama ngao wakati wa mashambulio yao hayo katika mji wa Lattakia.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imeeleza bayana kwamba kwa mtazamo wa Moscow hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni wa Israel  ni ya kiadui na imefanywa bila nadhari kwa makusudi, hivyo Russia inayo haki ya kutoa jibu dhidi ya hatua hiyo ya Tel Aviv.../

Tags

Maoni