• Mtumwa wa ngono mwenye umri wa miaka 16 kutoka Nigeria
    Mtumwa wa ngono mwenye umri wa miaka 16 kutoka Nigeria

Shirika la Kimataifa la Uhajiri (IOM) limetangaza kuwa, asilimia 80 ya wasichana wa Kinigeria wanaoingia Italia kupitia njia ya bahari wanatumiwa kama watumwa wa ngono.

Msemaji wa Shirika la Kimataifa la Uhajiri, Flavio Di Giacomo ameashiria wimbi kubwa la kuwatumia vibaya wahajiri katika masuala ya ngono na uasherati ili kukubaliwa huko Ulaya na kusema kuwa, wasichana wengi wa Afrika hususan kutoka Nigeria wamekuwa wahanga wa ukatili huo wa kingono. Ripoti iliyotolewa na shirika la OIM imesema kuwa, wakimbizi na wahajiri wanaoelekea katika nchi za Ulaya wanafungwa jela na kupewa mateso na wanalazimishwa kufanya kazi ngumu kwa miezi kadhaa bila ya kupewa malipo. 

Shirika la Kimataifa la Wahajiri pia amesema Nigeria na Libya zimefanywa soko la kuuza na kununua wahajiri.

Sera za nchi za kikoloni za Magharibi barani Afrika na kuvuruga amani na uchumi wa nchi hizo zinatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu za Waafrika wengi kulazimika kuhamia katika nchi za Ulaya kwa ajili ya kutafuta maisha bora.

 Wahamiaji hao wanakumbana na hatari nyingi wakiwa njiani kuelekea Ulaya ikiwa ni pamoja na kuuzwa kama watumwa hasa wa ngono na kazi ngumu, na wengi miongoni mwao wanapoteza maisha kwa kughariki bahari.   

Tags

Sep 19, 2018 03:46 UTC
Maoni