• Wabunge wa Umoja wa Ulaya wataka kutambuliwa rasmi nchi ya Palestina

Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wamezitaka nchi wanachama wa umoja huo kuitambua rasmi na haraka iwezekanavyo nchi huru ya Palestina.

Wabunge wa Kamati ya Uhusiano na Palestina ya Bunge la Ulaya jana walitoa taarifa rasmi na kutaka kuchukuliwa hatua za maana na umoja huo kwa ajili ya kuunga mkono haki ya wananchi wa Palestina kujiainishia mustakabali wao.

Wajumbe wa Kamati ya Uhusiano na Palestina ya Bunge la Ulaya siku ya Jumatatu walielekea Palestina kwa ajili ya kukitembelea kijiji cha Khan al-Ahmar kilichoko mashariki mwa Quds inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, uamuzi wa utawala haramu wa Israel wa kuataka kubomoa kijiji hicho cha Khan al Ahmar mashariki mwa mji mtakatifu wa Quds umeendelea kulaaniwa kila kona ya dunia.

Wapalestina wa kijiji cha Khan al-Ahmar na wanaharakati wa haki za binadamu katika juhudi za kuwazuia wanajeshi wa Israel wasibomoe nyumba za kijiji hicho

Nchi tano za Ulaya  za Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uhispania na Italia zimetangaza kuwa, zina wasiwasi na uamuzi huo wa utawala wa Kizayuni wa kutaka kubomoa kijiji cha Khan al Ahmar huko Quds na kusisitiza kuwa hatua hiyo itakuwa na taathira mbaya. 

Kijiji cha Khan al Ahmar kina umuhimu mkubwa kiistratijia hasa kwa kuzingatia kuwa, kijiji hicho kinayaunganisha maeneo ya mashariki mwa mji wa Quds Mashariki na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan hivyo Israel ina nia ya kukiteka na kukibomoa ili ipate kuyadhibiti maeneo hayo mawili ya Wapalestina.

Tags

Sep 21, 2018 04:01 UTC
Maoni