• Wabunge wa Kongresi ya Marekani wamtaka Trump atazame upya maamuzi yake dhidi ya watu wa Palestina

Wabunge 40 wa Kongresi ya Marekani wamemtaka rais wa nchi hiyo Donald Trump atazame upya maamuzi yake dhidi ya watu wa Palestina.

Katika ombi walilowasilisha kwa Trump, wabunge 34 wa Kongresi ya Marekani wamemtuhumu kiongozi huyo kuwa anajaribu kuidhoofisha Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) kwa kuwafukarisha na kuwakatisha tamaa watu wa Palestina.

Aidha wabunge wengine sita wamesaini barua ambayo ndani yake inamtuhumu rais wa Marekani kwamba anatumia siasa za kuwaweka na njaa watu wa Palestina kwa madhumuni ya kuwashinikiza viongozi wao waukubali mkataba uliopewa jina la "Muamala wa Karne."

Barua ya wabunge hao sita imebainisha kuwa kufungwa ofisi ya PLO mjini Washington kumedhihirisha kuwa serikali ya Marekani haiupi umuhimu wowote mchakato wa amani.

Katika barua yao hiyo wabunge wa Kongresi ya Marekani wameongeza kuwa, kwa hatua kadhaa ilizochukua serikali ya nchi hiyo, ikiwemo ya kuuhamishia Quds ubalozi wake wa Tel Aviv imeonyesha kwamba Washington haiwezi kuwa msuluhishi mzuri kwa ajili ya kufikiwa suluhu kati ya Wapalestina na Waisarel.

Kongresi ya Marekani

Itakumbukwa kuwa katika mchakato wa kufanikisha mpango wa "Muamala wa Karne", mnamo tarehe 6 Desemba 2017, Trump aliitangaza Quds tukufu kuwa mji mkuu wa utawala bandia wa Israel na tarehe 14 Mei mwaka huu akauhamishia kwenye mji huo ubalozi wa Marekani uliokuweko Tel Aviv.

Aidha katika miezi ya karibuni, serikali ya Trump imekata misaada yake ya fedha kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Ajira kwa ajili ya Wakimbizi wa Palestina UNRWA na kwa hospitali za mji wa Quds.../  

Tags

Sep 21, 2018 07:46 UTC
Maoni