Sep 22, 2018 16:43 UTC
  • Trump aitishia India pia kuiwekea vikwazo iwapo itanunua ngao ya S 400 ya Russia

Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kuiwekea vikwazo India, iwapo nchi hiyo itaendelea na azma yake ya kununua ngao ya makombora ya S 400 kutoka Russia.

Gazeti la The Economic Times linalochapishwa nchini India limeandika kuwa, utilianaji saini wa mauziano ya ngao hiyo ya makombora aina ya S 400 ya Russia, umepangwa kufanyika katika safari ya Rais Vladmir Putin mjini New Delhi, mwezi ujao. Viongozi wa India wametangaza kuwa, serikali ya nchi hiyo kamwe haitorudi nyuma katika azma yake ya kununua ngao hiyo ya makombora, kama ambavyo haitosalimu amri mbele ya matakwa ya Marekani. Kabla ya hapo Nirmala Sitharaman, Waziri wa Ulinzi wa India alinukuliwa akisema kuwa, huenda utilianaji saini huo kati ya New Delhi na Moscow, ukafanyika kabla ya safari ya Rais Vladmir Putin mjini New Delhi.

Trump aliyehamakishwa na hatua ya India ya kununua ngao ya S 400 ya Russia

Ngao ya makombora aina ya S 400, haijapata mshindani duniani ambapo nchi nyingi zinahitajia kununua silaha hiyo. Hivi karibuuni Rais Donald Trump wa Marekani alitia saini amri ambayo kwa mujibu wake nchi ambazo zitanunua ngao ya makombora ya S 400 kutoka Russia na zana nyingine za kijeshi, basi ziwekewe vikwazo na Washington. Nchi kama vile China, Russia na Uturuki zimetangaza wazi kutofuata maamuzi yoyote ya Trump.

Maoni