Sep 24, 2018 08:08 UTC
  • Mamia ya wahajiri waokolewa katika maji ya Uhispania

Jumuiya ya Misaada ya Uokoaji wa Baharini ya Hispania imetangaza kuwa, zaidi ya wahajiri 440 waliokuwa mbioni kuvuka Bahari ya Mediterrania na kuingia barani ulaya wameokolewa majini.

Jumuiya hiyo imetangaza kuwa, boti kadhaa zilizokuwa zimebeba wahajiri hao haramu zimeokolewa ikiwemo boti moja iliyokutwa katika maji ya karibu na kisiwa cha Majorca.

Idadi ya wahajiri haramu wanaoelekea Ulaya imeongezeka sana nchini Uhispania katika miezi ya hivi karibuni baada ya Italia kukataa kupokea wahajiri hao. Italia imesimamisha huduma zote za misaada ya kibinadamu kwa wahajiri wanaowasili pwani ya nchi hiyo, suala ambalo linawafanya wahajiri wengi kuelekea Uhispania. 

Maelfu ya wahajiri wamefariki dunia katika Bahari ya Mediterrania.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu zaidi ya wahajiri 300 waliokuwa mbioni kuelekea Uhispania pekee wamefariki dunia baada ya kuzama katika Bahari ya Mediterrania. Idadi ya wahajiri wote waliofariki dunia mwaka huu katika Bahari ya Mediterrania wakielekea Ulaya ni 1600. 

Tags

Maoni