Oct 16, 2018 14:10 UTC
  • UN yataka kuondolewa kinga ya kutoshtakiwa  wanadiplomasia wa Saudia wanaohusishwa na kadhia ya Khashoggi

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ametaka kuondolewa kinga ya kutoshtakiwa wanadiplomasia wa Saudi Arabia ambao inawezekana wamehusika na kutoweka nchini Uturuki, Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari raia wa Saudia.

Katika taarifa aliyotoa hii leo, Michelle Bachelet amesema, kwa kuzingatia uzito wa suala la kutoweka Jamal Khashoggi, kuna haja ya kufutwa marufuku ya kutofuatiliwa na kinga ya kutoshtakiwa inayotolewa kwa mwahala na wafanyakazi wake, ambazo zimetajwa kwenye mikataba kadhaa ukiwemo wa Vienna wa mwaka 1963.

Bi Bachelet aidha amezitaka Saudi Arabia na Uturuki ziweke hadharani taarifa zote zinazohusiana na kutoweka na pia zinazohusiana na uwezekano wa kuuawa Jamal Khashoggi.

Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa UN

Jamal Khashoggi, ambaye alikuwa mwandishi wa makala katika gazeti la Washington Post linalochapishwa nchini Marekani, tarehe Pili ya mwezi huu wa Oktoba alifika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki kwa ajili ya kufuatilia masuala ya kiofisi, lakini tangu wakati huo hadi sasa hakuna taarifa zozote kuhusiana na hatima yake.

Taarifa za awali za polisi ya Uturuki zinaonyesha kuwa Khashoggi aliuliwa ndani ya ubalozi huo mdogo wa Saudia mjini Istanbul.../

 

Tags

Maoni