Oct 22, 2018 08:15 UTC
  • Washington yalazimika kuzingatia msamaha kwa wanunuzi wa mafuta ya Iran

Waziri wa Fedha wa Marekani amelegeza msimamo wa nchi hiyo katika kuyawekea kikamilifu vikwazo mafuta ya Iran na kutangaza kuwa Washington inafikiria suala la msamaha kwa wanunuzi wa mafuta ya Iran.

Steven Mnuchin ameashiria namna msamaha huo utakavyotekelezwa na kubainisha kuwa nchi zinazonunua mafuta ya Iran ambazo zinapasa kupunguza kununua mafuta ya Iran kwa zaidi ya asilimia 20  kiwango  ambacho kilihitajika mwaka 2013 hadi 2015  ili kustafidi na msamaha huo wa Marekani. 

Mnuchini amekanusha kuwepo wasiwasi kuhusu kupanda bei ya mafuta kimataifa na kudai kuwa kupungua uzalishaji wa  mafuta ya Iran kumefidiwa. Waziri huyo wa Fedha wa Marekani amesisitiza pia kuwa uwezekano wa kupungua uzalishaji wa mafuta wa Iran umesababisha hali ya mvutano katika soko la kimataifa.

Steven Mnuchin, Waziri wa Fedha wa Marekani

Washington imechukua uamuzi wa kutekeleza msamaha kwa nchi zinazonunua mafuta kutoka Iran katika hali ambayo Rais Donald Trump wa Marekani siku kadhaa zilizopita alitilia mkazo mafuta ya Iran kuwekewa vikwazo kikamilifu na alidai kuwa ataurejesha uzalishaji wa mafuta ya nchi hii hadi kiwango cha sifuri. 

Duru ya kwanza ya vikwazo hivyo vya upande mmoja viliwekwa Agosti 7 na duru ya pili pia ambayo zaidi inajumuisha vikwazo vya mafuta inatazamiwa kutekelezwa Novemba nne mwaka huu. Pamoja na haya yote wanunuzi wakubwa wa mafuta ya Iran zikiwemo China na India zimetangaza kuwa zitaendelea kununua mafuta ya Iran.  

Tags

Maoni