Nov 11, 2018 12:46 UTC
  • Ukosoaji wa Korea Kaskazini dhdi ya uingiliaji wa Marekani katika uhusiano wa Korea mbili

Vyombo vya habari vilivyo karibu na serikali ya Korea Kaskazini, vimekosoa mpango wa Marekani wa kuanzisha jopokazi maalumu la kusimamia uhusiano wa Korea mbili na pia kufanya maneva za kijeshi za pamoja baharini.

Gazeti la Rodong Sinmun la chama tawala sambamba na kukosoa vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi hiyo, limeandika kuwa jopokazi la pamoja kati ya Washington na Seoul ni kizuizi kikubwa katika njia ya kuboresha uhusiano wa Korea mbili, kama ambavyo pia ni uingiliaji wa moja kwa moja wa Washington katika eneo. Inafaa kuashiria kuwa, wiki iliyopita Korea Kusini na Marekani ziliunda jopokazi la kufanya kufuatilia kwa karibu vikwazo vya Korea Kaskazini, kuifanya Peninsula ya Korea kutokuwa na silaha za atomiki na kudumisha usalama wa eneo. Ukosoaji wa Korea Kaskazini dhidi ya Marekani unatokana na uingiliaji wake katika masuala ya ndani ya Korea mbili na ambao umetajwa na nchi hiyo kuwa mwenendo hasi wa White House kuhusiana na mipango iliyowekwa kati ya Seoul na Pyongyang kwa ajili ya kupunguza mzozo na kurejesha uhusiano wa kirafiki katika nyanja tofauti za ushirikiano wa pande mbili.

Uhusiano mwema wa Korea mbili waikera Marekani

Baada ya kuanza mazungumzo ya Korea Kusini na Marekani kwa upande mmoja na Korea Kaskazini kwa upande wa pili, kwa ajili ya kutatua tofauti za pande mbili, mazungumzo ya Seoul na Pyongyang yalichukua mkondo chanya, kinyume na yalivyokuwa yale ya Korea Kaskazini na Marekani. Hii ni kwa kuwa kupenda makubwa kwa Washington, kuendeleza hatua za kichochezi za nchi hiyo kukiwemo kuendelezwa vikwazo dhidi ya Pyongyang na kadhalika kuendelezwa tuhuma za viongozi wa White House dhidi ya nchi hiyo ya Asia kwamba haijafanya juhudi za kutosha kwa ajili ya kusimamisha miradi yake ya nyuklia, ni mambo yaliyopelekea mazungumzo kati ya pande mbili hizo kuendelea kutoaminiana. Wasi wasi wa mazungumzo ya Korea mbili kuzaa matunda ya kuridhisha na hivyo kuipelekea Seoul kulegeza misimamo kuhusiana na Pyongyang, umeifanya White House kuunda jopo kazi la pamoja na Korea Kusini ili itie dosari katika mazungumzo ya hayo. Katika uwanja huo, Andrew Ivanov, mtaalamu wa ngazi ya juu wa nchini Russia na muhadhiri wa masuala ya uhusiano wa kimataifa anasema: “Kila mara anga nzuri inapoandaliwa kwa ajili ya kupatikana amani katika eneo la Korea, Marekani huibua tuhuma na matakwa mapya, suala ambalo huwa linalenga kukwamisha kufikiwa makubaliano katika eneo hilo.” Mwisho wa kunukuu.

Marekani na njama zake chafu za kuilaghai Korea Kusini

Katika mkondo wa siasa hizo za Marekani ambazo kimsingi zinalenga kuvuruga uhusiano wa Seoul na Pyongyang, hivi karibuni kulifanyika maneva ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini kwa lengo la kuishinikiza Pyongyang, maneva ambayo hata hivyo yalikabiliwa na radiamali kali ya Korea Kaskazini. Aidha hatua ya viongozi wa Washington ya kuchochea hisia za Korea Kaskazini kwa kufanya maneva ya pamoja kati ya Marekani, Korea Kusini na Japan katika eneo, inalenga kutia dosari mazungumzo ya Korea mbili. Ni kwa msingi huo ndio maana serikali ya Pyongyang ikaingiwa na wasi wasi kuhusiana na uingiliaji wa Marekani katika uhusiano wa Korea mbili na taathira zake haribifu kwenye mipango ya amani ya Seoul na Pyongyang. Katika hali hiyo viongozi wa Korea Kaskazini wanataraji kuwaona viongozi wa Korea Kusini wakizingatia maslahi yao ya kitaifa na kieneo bila kuathiriwa na mashinikizo ya Marekani.

Tags

Maoni