Dec 09, 2018 02:53 UTC
  • Trump akejeli maandamano ya Ufaransa, asema eti Wafaransa wanataka rais kama yeye

Katika kile kinachoonekana ni kukejeli maandamano ya wananchi wa Ufaransa wanaopinga mfumo wa kibepari, rais wa Marekani Donald Trump amedai kuwa maandamano hayo ni ya kuunga mkono siasa zake za mazingira na tabianchi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Trump jana Jumamosi aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, makubaliano ya mazingira ya Paris yameshindwa kufanya kazi inayotakiwa na ndio maana maandamano yameenea katika kona zote za Ufaransa.

Rais huyo wa Mrekani vile vile amedai kuwa, wananchi wa Ufaransa wanapinga suala la kulindwa mazingira na eti kama Wamarekani nao pia wanataka rais kama Trump.

Maandamano ya wavaa vijambakoti vya njano nchini Ufaransa

 

Madai hayo ya Donald Trump yametolewa katika hali ambayo uchunguzi wa hivi karibuni wa maoni unaonesha kuwa, kiwango cha Wamarekani wanaochukia siasa zake ni kikubwa zaidi hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote.

Tofauti kabisa na madai hayo ya Trump, maandamano ya wananchi wa Ufaransa hayana uhusiano wowote na mazingira, bali ni ya kupinga siasa za serikali ya Paris za kuongeza ushuru wa mafuta na vile vile kupinga mfumo wa kibepari.

Hatua ya Trump ya kuitoa Marekani katika Mkataba wa Kulinda Mazingira wa Paris mwaka jana 2017 inaendelea kulaaniwa hadi leo hii ndani na nje ya nchi hiyo.

Tags

Maoni