Dec 09, 2018 02:53 UTC
  • Ujerumani yapinga kuongezwa vikwazo vya nchi za Ulaya dhidi ya Russia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumaini amegusia mapigano ya hivi karibuni baina ya Russia na Ukraine na kusema kuwa suala la kuongeza vikwazo vya nchi za Ulaya dhidi ya Moscow haliingii akilini.

Heiko Maas alisema hayo jana Jumamosi katika mahojiano na shirika la habari la Reuters na kuongeza kuwa, suala la kuiwekea vikwazo vingine Russia hivi sasa si la mantiki hata kidogo.

Amesema, kuweka vikwazo vipya dhidi ya Moscow hauwezi kuwa uamuzi mzuri wa kukabiliana na nchi hiyo.

Msuguano baina ya Russia na Ukraine katika Bahari Nyeusi

 

Tarehe 25 Novemba mwaka huu, meli tatu za kijeshi za Ukraine ziliingia katika mipaka ya majini ya Russia katika Lango Bahari la Kerch na kujibiwa vikali na haraka sana na jeshi la Russia. Mbali na kuzikamata meli hizo, wanajeshi wa Russia waliwaweka kizuizini wote waliokuwemo kwenye meli hizo za Ukraine.

Suala hilo linataka kutumiwa vibaya na Marekani kuishinikiza zaidi Russia kiasi kwamba hivi karibuni Washington iliwasiliana na maafisa wa nchi za Ulaya wa Jeshi la Nchi za Magharibi NATO na kuwataka waunge mkono kampeni ya kuiwekea vikwazo vipya Russia.

Hata hivyo Ujerumani imetangaza wazi kupinga jambo hilo na inasema kuwa kuiwekea vikwazo vipya Russia si jambo la mantiki hata kidogo kwa hivi sasa.

Tags

Maoni