Dec 09, 2018 07:21 UTC
  • China yaionya Canada kuhusu kumpeleka Marekani mkuu wa Huawei

Serikali ya China imetoa onyo kali na kuitaka Canada imuachie huru mara moja mkuu wa shirika kubwa la mawasiliano la Huawei na isithubutu kumkabidhi kwa wakuu wa mahakama za Marekani.

Taarifa yya Wizara ya Mambo ya Nje ya China imeitaka Canada imuachie huru Bi. Meng Wanzhou Mkurugenzi wa Masuala ya Fedha katika shirika la Huawei na kuhakikisha haki zake za kisheria zinalindwa la sivyo Canada itabeba dhima ya matokeo mabaya ya kadhia hiyo. Balozi wa Canada mjini Beijing ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China na kukabidhiwa malalamiko kuhusuana na suala hilo.
Wanzhou alikamatwa Disemba Mosi kufuatia ombi la Marekani wakati akiwa katika uwanja wa ndege mjini Vancouver, Canada. Meng ambaye ni bintiye mwanzilishi na mmili wa kampuni ya Huawei, Ren Zhengfei, anatajwa kuwa mrithi mtarajiwa wa msimamizi wa shirika hilo. Alikamatwa kwa tuhuma kuwa shirika la Huawei, kupitia shirika lingine, limekiua vikwazo vya Marekani kwa kuuiuzuia Iran vifaa vya mawasiliano. 

Kukamatwa mkuu wa Huawei Canada kunatajwa kuwa ni sehemu ya vita dhidi ya bidhaa za teknolojia za shirika hilo ambazo zimepata umashuhuri duniani

Mahakama ya Canada Jumatatu ya kesho itasikiliza ombi la Marekani la kutaka ikabidhiswe Mengi ili apandishwe kizimbani Marekani. Iwapo atapatikana na hatia, Meng anaweza kufungwa jela miaka 30. 
Shirika la Huawei limekuwa chini ya mashinikizo makubwa ya madola ya Magharibi kwa tuhuma kuwa linafanya ujasusi kwa niaba ya serikali ya China.

Weledi wa mambo wanaamini kuwa mashinikizo dhidi ya Huawei ni sehemu ya vita vya kibiashara vya Marekani na nchi za Magharibi ambazo zinalenga kupunguza satwa na ushawishi wa China kiuchumi hasa katika uga wa teknolojia.

Tags

Maoni