Dec 12, 2018 07:32 UTC
  • Republican yaikosoa Google kwa 'kuanika upumbavu wa Trump'

Mbunge wa chama cha Rebublican nchini Marekani amemjia juu Ofisa Mkuu Mtendaji wa shirika la intaneti la Google, na kumtaka afafanue kwa nini kila akitafuta neno 'mpumbavu' kwenye mtandao huo, picha zinazokuja ni za Rais Donald Trump.

Mbunge wa Texas wa chama cha Republican nchini Marekani, Lamar Smith amesema anaitakidi kuwa kuna uwezekano mkubwa na ni jambo linaloyumkinika kubadilisha matokeo ya majina yanayotafutwa kwenye mtandao huo.

Katika kikao cha jana Jumanne cha kujadili masuala ya faragha na ukusanyaji wa data kwenye mtandao wa intaneti, Zoe Lofgren, mwakilishi wa California wa chama cha Democrats alimtaka ofisa huyo mwandamizi wa Google kufafanua, "Kwa nini kila unapotafuta neno pumbavu kwenye Google, picha zinazokuja kwa wingi ni za Trump? Hili linafanyikaje? Mnatumia mbinu zipi kufikia hili?"

Trump aongoza katika orodha ya mashine ya utafutaji ya google kwa jina la "idiot" mpumbavu

 

Hata hivyo Sundar Pichai, Ofisa Mkuu Mtendaji wa shirika la intaneti la Google la Marekani amekanusha vikali madai ya Warepublican kwamba huenda Google imewaagiza wafanyakazi wake kubadilisha baadhi ya matokeo ya majina yanayotafutwa kwenye mtandao huo kwa maslahi ya misimamo na mielekeo fulani ya kisiasa.

Hii ni katika hali ambayo, mwishoni mwa mwaka uliopita, matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanyika nchini Marekani yalionesha kuwa, neno "mpumbavu" ndilo linaloingia katika bongo na fikra za Wamarekani wengi baada ya kusikia jina la Rais wa nchi hiyo, Donald Trump.

Idadi kubwa zaidi ya watu walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni uliosimamiwa na Chuo Kikuu cha Quinnipiac walisema kuwa, neno la kwanza kabisa linaloingia akilini mwao baada tu ya kusikia jina la Donald Trump ni "mpumbavu".

Tags

Maoni