Dec 13, 2018 08:13 UTC
  • Seneta wa Marekani: Bin Salman anapasa kutangazwa kuwa muuaji wa Khashoggi

Kiongozi wa waliowengi katika Seneti ya Marekani amesema kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia ndiye aliyemuuwa mwandishi habari na mkosoaji wa utawala wa Aal Saud.

Mitch MacConnell amesema kuwa seneti ya Marekani inapasa kuunga mkono azimio ambalo litamuarifisha Muhammad bin Salman Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia kuwa mhusika wa mauaji ya Jamal Khashoggi mwandishi habari mkosoaji wa utawala wa Aal Saud.  

Jamal Khashoggi alitoweka tarehe Pili mwezi Oktoba mwaka huu baada ya kuingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Uturuki na hatimaye Saudi Arabia kutokana na mashinikizo ya kimataifa, ilithibitisha kuwa mwandishi huyo wa habari aliuawa akiwa ndani ya ubalozi wa nchi hiyo.

Mwendazake Jamal Khashoggi akiingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Uturuki mnamo Oktoba Pili 

Vyombo vya habari kwa kutegemea ripoti iliyotolewa na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) vimearifu kuwa, Jamal Khashoggi aliuliwa kwa agizo la moja kwa moja la Muhammad bin Salman hata hivyo serikali ya Marekani hadi sasa imejizuia kuichukulia hatua serikali ya Saudi Arabia bali imefanya jitihada za kuunga mkono mikataba mikubwa ya kijeshi kati yake na Riyadh. 

Maoni