Dec 15, 2018 02:50 UTC
  • Machafuko ya Ufaransa yameshafika pia Uingereza

Makumi ya watu wanaounga mkono maandamano ya wananchi wa Ufaransa wanaolalamikia matatizo ya kiuchumi na mfumo wa kibepari wamefanya maandamano mjini London Uingereza na kukwamisha shughuli za kila siku mjini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, waandamanaji hao jana Ijumaa waliandamana katika eneo la Westminster la katikati mwa London karibu na Bunge la Uingereza na kufunga njia suala ambalo lilikwamisha harakati za kawaida katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti hiiyo, kundi hilo la waandamanaji lilizuia mabasi na magari kupita kwenye njia hiyo.

Waandamanaji hao walikuwa wakipiga nara za kuitaka Uingereza itoke karaka kwenye Umoja wa Ulaya na bila ya hata kufanya mazungumzo.

Maandamano ya kupinga ubepari na hali ngumu ya maisha katika nchi ya Ulaya ya Ufaransa. Polisi wanakandamiza kikatili maandamano ya wavaa vizibao vya njano nchini humo

 

Wapinzani wa mfuno wa kiuchumi na wa kibepari ambao wamepata umaarufu wa jina la "wavaa vizibao vya njano" wamekuwa wakifanya maandamano makubwa kwa karibu mwezi mzima sasa nchini Ufaransa. Maandamano hayo yameshafika hadi katika nchi nyingine kadhaa za Ulaya kama vile Uingereza, Ubelgiji na Uholanzi.

Serikali ya Ufaransa inalaumiwa kwa kuwakandamiza kikatili waandamanaji kama ambavyo mashirika yanayojifanya kupigania haki za binadamu duniani nayo yanalaaniwa kwa kunyamazia kimya ukandamizaji huo, wakati mashirika hayo yanavalia njuga kupindukia matukio mengine madogomadogo tu yanayotokea katika nchi zisizo waitifaki wa madola ya Magharibi.

Tags

Maoni