Dec 17, 2018 02:39 UTC
  • Marekani inazidi kudhoofika kimataifa, Russia na China zinaimarika

Mchambuzi na mtaalamu maarufu wa masuala ya kisiasa wa chama cha Republican amekiri kuwa Marekani inazidi kudhoofika katika uga wa kimataifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Sputnik, Patrick Buchanan mchambuzi maarufu wa masuala ya kisaisa Marekani ameandika katika makala kuwa, Russia na China zinazidi kuimarika na kupata nguvu zaidi huku Marekani ikidhoofika katika nyuga mbali mbali. Aidha amesema madai ya Marekani kuwa eti ni mtetezi mkuu wa demokrasia duniani sasa hayatiliwi maanani tena. Buchanan ameendelea kusema kuwa, waliowengi duniani wana mtazamo hasi kumhusu Rais Donald Trump wa Marekani na sera za utawala wake.

Sera za Trump ambazo zimewakasirisha walimwengu ni pamoja na maamuzi yake ya upande mmoja ya kiuchumi na kujiondoa katika mikataba muhimu ya kimataifa.

Meli ya kivita ya China yenye uwezo wa kusheheni ndege

Wakati huo huo Kituo cha Tathmini ya Kistratejia na Bajeti (CSBA) chenye makao yake mjini Washington kimeripoti kuwa manowari za kivita za Marekani sasa zinakumbwa na changamoto kubwa katika kukabiliana na madola makubwa kama vile China na Russia.

 

Tags

Maoni