Feb 15, 2019 07:39 UTC
  • UN yalaani shambulio la kigaidi la kusini mashariki mwa Iran

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa na kulaani shambulio la kigaidi lililotokea Jumatano usiku katika mkoa wa Sistan na Baluchistan wa kusini mashariki mwa Iran.

Kwa mujibu wa televisheni ya al Alam, taarifa hiyo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imesema, wanachama 15 wa baraza hilo wamesikitishwa mno na wanatoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa shambulio hilo na kwa serikali ya Iran.

Kabla ya hapo msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alikuwa amelaani shambulizi la kigaidi lililotokea Jumatano kusini mashariki mwa Iran na alikuwa ametoa mkono wa pole kwa wafiwa na kwa serikali ya Iran.

Sehemu lilipotokea shambulizi la kigaidi kusini mashariki mwa Iran

Stéphane Dujarric alitoa mkono huo wa pole jana Alkhamisi wakati akijibu swali la mwandishi wa shirika la habari la IRNA aliyetaka kujua msimamo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu shambulio la kigaidi la siku ya Jumatano lililotokea nchini Iran ambalo limefanywa na genge la kigaidi linaloungwa mkono na nchi zilizoitisha kikao cha Warsaw Poland dhidi ya Iran. Dujjaric amesema, msimamo wa Umoja wa Mataifa ni kulaani kitendo chochote kile cha kigaidi kikiwemo kilichotokea nchini Iran siku ya Jumatano.

Stéphane Dujarric

 

Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, tunalaani shambulio la kigaidi lililotokea katika mkoa wa Sistan va Baluchistan nchini Iran na tunatoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa shambulio hilo pamoja na kwa serikali ya Iran na tunawaombea dua majeruhi waweze kupona haraka.

Genge la kigaidi na la ukufurishaji  linalojiita Jaishul Adl limetoa taarifa likitangaza kuwa ndilo lililofanya jinai na mauaji hayo. Kundi hilo lenye itikadi na fikra za kisalafi na Kiwahabi ni miongoni mwa magenge yanayoshirikiana na makundi ya ukufurishaji na kigaidi huko Syria. 

Hadi sasa kundi hilo limetangaza kuhusika na mauaji kadhaa ya kigaidi katika mkoa wa Sistan va Baluchestan kusini mashariki mwa Iran likiwemo shambulizi lililoua walinda mipaka 9 katika eneo la Mirjaveh tarehe 26 Aprili mwaka 2017. 

Tags

Maoni