Feb 21, 2019 02:54 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Uingereza: Kulindwa  JCPOA ni nukta muhimu katika uhusiano wa nchi hiyo na Ujerumani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amesema kuwa kuyalinda makubaliano ya nyuklia ya JPOA ni moja ya nukta muhimu katika uhusiano kati ya London na Berlin baada ya Uingereza kuondoka ndani ya Umoja wa Ulaya.

Akizungumza mjini Berlin jana Jumatano, Jeremy Hunt  Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amebainisha kuwa London na Berlin zina nukta nyingi za pamoja na kwamba pande mbili zitayalinda makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kwa kushirikiana. Umoja wa Ulaya umeanza kuchunguza mipango mbadala kwa lengo la kulinda miamala ya kibiashara kati yake na Iran baada ya Marekani kujitoa katika makubaliano hayo ya kimataifa ya nyuklia mwaka uliopita.  

Jeremy Hunt, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza

Hunt ametaka kuendelezwa uhusiano wa London na Berlin hata baada ya Uingereza kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya. Iran na upande wa Ulaya zimekuwa zikifanya mazungumzo katika miezi ya karibuni lengo lake likiwa ni kuhakikisha kuwa makubaliano ya JCPOA yanalindwa baada ya kujitoa Marekani. Hatimaye tarehe 31 mwezi Januari mwaka huu baada ya kupita miezi kadhaa; Ulaya ilitangaza rasmi kuanzisha kanali maalumu ya uendeshaji biashara na Iran kwa jina la INSTEX. 

Tags

Maoni