Mar 20, 2019 16:27 UTC
  • Venezuela: Tutatumia nguvu kali kukabiliana na vitisho vipya vya kijeshi vilivyotolewa na Trump

Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela ametoa radiamali kali juu ya vitisho vipya vya kijeshi vilivyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya nchi yake na kusisitiza kwamba, Caracas inapinga vikali matamshi hayo hatari ya Trump.

Jorge Arreaza ametoa radiamali hiyo akijibu matamshi ya Trump aliyoyatoa alipokutana na Rais Jair Bolsonaro wa Brazil na kusema kuwa serikali ya Venezuela inapinga vikali vitisho vya marais hao wa Marekani na Brazil. Taarifa hiyo imeongeza kwamba serikali ya Caracas na katika kuanzisha eneo la amani huko Amerika ya Latini na bahari ya Caribbean, inafungamana na sheria za kimataifa. Jumanne usiku Rais Donald Trump, akiwa na Rais Jair Bolsonaro wa Brazil ndani ya ikulu ya Marekani (White House), wakati akijibu swali la mwandishi wa habari juu ya uwezekano wa Marekani kuingilia kijeshi nchini Venezuela, alikariri tena vitisho vya kila mara kwamba machaguo yote yako mezani.

Jorge Arreaza, Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela

Kukaririwa vitisho vya Trump kwamba huwenda akatumia chaguo la kijeshi dhidi ya Venezuela, na kadhalika uungaji mkono wake kwa Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani aliyejitangaza kuwa rais wa muda wa nchi hiyo kunajiri katika hali ambayo jeshi na wananchi wameendelea kushikamana na Rais Nicolás Maduro aliyechaguliwa kisheria. Aidha Rais wa Brazil ambaye misimamo yake ni sawa na ya Marekani, amesisitizia umuhimu wa kumuunga mkono Guaidó, Hayo yanajiri katika hali ambayo nchi nyingi kama vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia, China, Italia, Afrika Kusini, Chuba n.k, zimetangaza kuiunga mkono serikali halali ya Rais Nicolás Maduro, sambamba na kupinga aina yoyote ya uingiliaji wa kigeni katika masuala ya ndani ya Venezuela.

Tags

Maoni