Apr 26, 2019 04:42 UTC
  • Ukosoaji wa Rais Vladmir Putin kuhusiana na miamala mibovu ya Marekani kimataifa

Siasa za upande mmoja za Rais Donald Trump wa Marekani, zimeibua mizozo mingi katika ngazi za kimataifa.

Trump kupitia nara yake ya 'Marekani Kwanza' anadai kwamba siasa zake za upande mmoja na za umimi, zitaweza kuifanya Washington kuwa yenye nguvu na kuwashinda washindani wake kimataifa. Madola yenye nguvu duniani na ambayo ni washindani wakubwa wa Marekani hususan Russia, zimeonyesha upinzani mkali kwa mienendo hiyo ya kujichukulia hatua za upande mmoja za Marekani sambamba na kukataa utwishaji mambo unaofanywa na serikali ya Trump. Katika fremu hiyo Rais Vladmir Putin wa Russia kupitia ujumbe alioutoa kwenye kongamano la nane la Usalama wa Kimataifa mjini Moscow ameelezea matokeo mabaya na hatari yanayotokana na mienendo hiyo ya Marekani katika ngazi za kimataifa. Kuhusiana na suala hilo "Sambamba na kutangaza kwamba muundo wa vita baridi sasa umefikia ukingoni amesema kuwa, mienendo ya Marekani inaharibu uthabiti na kuhatarisha usalama wa dunia na kwamba baadhi ya mashinikizo ya kiuchumi yanayowekwa dhidi ya nchi nyingine yanakiuka sheria za kimataifa." Maneno ya Rais Putin yanalenga moja kwa moja siasa na misimamo hasi ya Rais Donald Trump wa Marekani ambaye amekuwa akijitapa kuhusu ubora wa nchi yake na kuzilazimisha nchi nyingine kufuata siasa za Washington kwa maslahi ya Marekani.

Pande tatu ovu ambazo zinahusika na kuchafua anga ya maelewano kote duniani

Wakati huo huo Trump amekuwa akiiondoa nchi yake kwenye makubaliano ya kimataifa suala ambalo limekuwa na matokeo mabaya zaidi kwa ajili ya uthabiti na usalama wa dunia. Kuhusiana na suala hilo, Sergey Shoygu, Waziri wa Ulinzi wa Russia kwenye mkutano wa nane wa Usalama wa Kimataifa mjini Moscow, sambamba na kuashiria hatua ya kujiondoa serikali ya Washington katika makubaliano mbalimbali ya kimataifa amesema: "Kujiondoa Marekani kwenye mkataba wa kuzuia silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati kwa kifupi INF na kadhalika makubaliano ya nyukklia ya Iran (JCPOA) kunaonyesha wazi kutoheshimiwa na Marekani makubaliano wala sheria za kimataifa." Hivi sasa Marekani inakabiliana na madola mawili yenye nguvu ambayo ni Russia na China ambapo katika nyuga mbalimbali madola hayo yameisababishia changamoto nyingi serikali ya Washington. Huku akidai kwamba washindani wake hao wanatumia vibaya urafiki wao na Marekani, Trump anasisitizia umuhimu wa kubadilishwa mienendo hiyo. Kwa hakika mienendo ya Trump ina maana ya kuendelea kushtadi juhudi za serikali yake katika kuzitwisha nchi nyingine matakwa yake binafsi hususan nchi washindani na maadui wake na hata marafiki wake pia.

Ubeberu na mabavu ya Marekani dhidi ya nchi nyingine za dunia

Pamoja na hayo viongozi wengi wa nchi kubwa za dunia wakiwemo wa nchi washirika wa Ulaya, nao pia wameonyesha wasi wasi mkubwa kuhusiana na siasa mbovu zinazotekelezwa na Rais Donald Trump na kwamba siasa hizo zitapelekea kutengwa na kutoaminiwa tena Marekani. Kuhusiana na suala hilo, Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amesema: "Trump aliyeingia ikulu ya Marekani kwa nara ya 'Marekani Kwanza', hivi sasa ameenda mbali zaidi kwa kufuata nara ya 'Marekani Pekee'. Yaani kwamba sasa Marekani itafchochea vita na mizozo katika kila pembe na kufanya mazungumzo yenye kuzingatia maslahi yake binafsi." Marekani ambayo inajiona kuwa polisi wa dunia, imejitwisha jukumu la kufuatilia masuala mbalimbali ya dunia kupitia nguvu za kijeshi na mabavu ya kiuchumi. Kuhusiana na suala hilo Valery Gerasimov, Mkuu wa Majeshi ya Russia anasema: "Marekani inaendeleza siasa za vikwazo ili kwa njia hiyo iweze kuzilazimisha nchi nyingine kutekeleza matakwa yake." Matukio ya kimataifa, yanaonyesha kwamba kimsingi mwenendo wa Marekani hauzingatii uhalisia wa mambo kuhusiana na sheria za kimataifa. Aidha mienendo na hatua za rais wa Marekani zitapelekea kuongezeka hali ya kutengwa na kuchukiwa zaidi nchi hiyo katika nyuga za kimataifa suala ambalo litatoa pigo kubwa kwa Washington.

Tags

Maoni