Apr 26, 2019 04:49 UTC
  • Korea Kaskazini yatoa radiamali kali kwa maneva ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini

Serikali ya Korea Kaskazini imetoa radiamali kali kufuatia maneva ya kijeshi ya hivi karibuni kati ya Marekani na Korea Kusini katika Rasi ya Korea.

Alkhamisi ya jana Kamati ya Umoja inayoshughulikia masuala ya umoja wa Korea mbili ya upande wa Korea Kaskazini sambamba na kulaani hatua ya Korea Kusini na Marekani ya kufanya luteka ya pamoja ya kijeshi ya majeshi yao ya anga katika eneo hilo, ilisema kuwa jeshi la Korea Kaskazini litatoa jibu mkabala kwa jirani yake huyo kuhusiana na harakati hizo za kijeshi. Taarifa hiyo ilimeweka wazi kwamba, viongozi wa Korea Kusini wameenda kinyume na maridhiano ya pande mbili na kwamba harakati hizo zimeikatisha matumaini serikali ya Pyongyang.

Maneva hayo ya pamoja kati ya majeshi ya Korea Kusini na Marekani

Aidha taarifa hiyo imesisitiza kwamba, maonyesho hayo ya kijeshi ya pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini katika Rasi ya Korea, yamekiuka makubaliano ya kijeshi ambayo yalifikiwa katika kikao cha viongozi wa nchi mbili mwezi Septemba mwaka jana. Kuanzishwa kamisheni ya kijeshi kwa ajili ya kuzidisha hali ya kuaminiana kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini na pia kuanzishwa eneo la mpakani katika Bahari ya Njano na Bahari ya Japan kwa ajili ya maneva huru, ni baadhi ya vipengee vya makubaliano ya mwezi Septemba mwaka jana yaliyofikiwa kati ya Kim Jong-un wa Korea Kaskazini na Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini mjini Pyongyang.

Tags

Maoni