Apr 26, 2019 04:49 UTC
  • New Zealand yasisitiza kwamba miripuko ya Sri Lanka haina mahusiano na hujuma za Christchurch

Ofisi ya Waziri Mkuu nchini New Zealand imetupilia mbali madai ya viongozi wa Sri Lanka kwamba mashambulizi ya kigaidi ya hivi kaibuni mjini Colombo, mji mkuu wa nchi hiyo, yana mahusiano na hujuma za kigaidi za mwezi Machi mjini Christchurch.

Taarifa hiyo imetolewa na ofisi ya Waziri Mkuu nchini New Zealand ikiwa ni radiamali kwa matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Sri Lanka ambaye alidai kwamba miripuko hiyo ya kigaidi mjini Colombo ina mahusiano na hujuma ya kigaidi iliyotokea tarehe 15 Machi mwaka huu dhidi ya Waislamu waliokuwa wakiswali ndani ya misikiti miwili ya mji wa Christchurch. Taarifa hiyo imeongeza kwamba matokeo ya uchunguzi wa kwanza uliofanywa na vyombo vya usalama nchini Sri Lanka kuhusiana na mashambuli ya hivi karibuni, hayana uhusiano na yale yaliyofanywa nchini New Zealand.

Baadhi ya magaidi wanaodhaniwa kuhusika na hujuma ya nchini Sri Lanka

Kabla ya Ruwan Wijewardene, Waziri wa Ulinzi wa Sri Lanka kufutwa kazi alidai kwamba, kwa mujibu wa uchunguzi wa awali uliofanywa kuhusiana na miripuko ya kigaidi iliyotokea ndani ya makanisa na hoteli kadhaa mjini Colombo, kuna uhusiano na hujuma za kigaidi zilizotokea katika misikiti miwili nchini New Zealand na kwamba wahusika wake ni watu walikuwa na lengo la ulipizaji kisadi kufuatia hujuma za mwezi jan, jambo ambalo limetupiliwa mbali na viongozi wa New Zealand. Jumapili iliyopita, ya tarehe 21 Aprili kulijiri miripuko kadhaa ya kigaidi katika makanisa na hoteli mjini Colombo ambapo kwa akali watu 359 waliuawa na wengine zaidi ya 500 kujeruhiwa. Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) limetangaza kuhusika na hujuma hiyo. 

Maoni