Aug 12, 2018 15:14 UTC

Siku ya Jumatano ya tarehe 8 Agosti 2018 Tanzania na eneo zima la Afrika Mashariki na Kati lilikumbwa na msiba wa kuondokewa na msanii mkongwe wa filamu hasa za vichekezo, mzee Amri Athumani, maarufu kwa jina la Mzee Majuto au King Majuto kama wanavyomuita mashabiki wake.

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na viongozi wengine wa ngazi za juu akiwemo Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubaka Zuberi bin Ally waliongoza waombolezaji katika shughuli ya maziko ya msanii huyo. Mwenyezi Mungu ailaze mahala pema roho ya mzee Amri Athumani, maarufu kwa jina la Mzee Majuto, na sisi tuliobakia asituondoe dunia ila baada ya kuwa radhi nasi, Aamin. Hapa tumekuwekeeni kipindi cha Afrika Wiki hii ambacho sehemu yake kubwa ilizungumzia kifo cha gwiji huyo katika tasnia ya filamu Afrika Mashariki.

Tags

Maoni