Makala Mchanganyiko

 • Pamoja na Imam Hasan al Mujtaba AS (kwa mnasaba wa siku ya kuzaliwa kwake)

  Jun 10, 2017 03:10

  Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum wapenzi wasikilizaji. Mwezi 15 Ramadhani ni siku inayosadifiana na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Imam Hasan al Mujtaba, mjukuu mpenzi wa Bwana Mtume Muhammad SAW.

 • Nyendo za Mtume SAW katika maisha ya Imam Khomeini MA

  Jun 05, 2017 09:27

  Assalaam Alaykum wasikilizaji wapenzi, karibuni kujiunga nami kwenye kipindi hiki maalumu ambacho kimetayarishwa kwa mnasaba wa kukumbuka siku ya kufariki dunia Imam Ruhullah Mussawi al Khomeini (MA) mwasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Ni matumaini yangu kuwa mtakuwa nami hadi tamati ya kipindi hiki, karibuni.

 • Mambo ya kujichunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani

  Jun 01, 2017 05:46

  Assalamu alaykum warahmatullahi wabarakatuh. Karibuni wasikilizaji wapenzi katika kipindi hiki maalumu nilichokuandalieni kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambacho kwa leo kitaanza kwa kugusia falsafa na hekima ya funga.

 • Maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa Imam Mahdi AS

  May 12, 2017 03:58

  Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum wasikilizaji wapenzi na karibuni katika kipindi hiki maalumu tulichokuandalieni kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Imam Mahdi AS. Tunaianza makala hii fupi kwa kusema: Nuru ya umaanawi ya uwepo wa Imam Mahdi AS imeenea hata katika wakati huu wa "ghaiba" wa kutokuwepo mtukufu huyo machoni mwa walimwengu.

 • Makala maalumu kwa mnasaba wa kukumbuka siku ya kuzaliwa Imam Sajjad AS

  May 01, 2017 09:52

  Assalaam Alaykum wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika dakika hizi chache za kipindi hiki maalumu ambacho kinakujieni kwa mnasaba wa kukumbuka siku ya kuzaliwa Imam Ali bin Hussein Zainul Abidiin AS mmoja kati ya Watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume Muhammad SAW.

 • Abul Fadhl Abbas AS, shujaa muungwana

  Apr 30, 2017 17:57

  Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum. Tuko katika siku ya kukumbuka kuzaliwa Hadhrat Abul Fadhl Abbas AS na tunawakaribisha kusikiliza makala hii maalumu ambayo tumekutayarishieni kwa mnasaba wa kukumbuka siku ya kuzaliwa Abul Fadhlil Abbas, mwana wa Imam Ali AS na ambaye alikuwa jemedari shujaa na nguzo muhimu ya Imam Hussein AS katika mapambano ya Karbala.

 • Iran, nchi ya tatu kuidhaminia Iraq mahitaji yake ya msingi

  Apr 30, 2017 01:20

  Licha ya kuwepo historia chungu ya vita vya kulazimishwa baina yao, lakini nchi mbili jirani za Iran na Iraq hivi sasa zimefungua ukurasa mpya wa mashirikiano.

 • Imam Hussein AS, kigezo bora kwa wapigania ukombozi

  Apr 29, 2017 12:53

  Tarehe tatu Shaaban ni kumbukumbu ya kuzaliwa shakhsia mkubwa ambaye aliyapa maana kamili maneno ya umaridadi na mapenzi. Ana moyo maridadi, karama, maarifa ya kina na hatimaye yeye ni kielelezo cha maisha ya mwanaadamu aliyekamilika. Leo ni siku ambayo mji wa Madina ulishuhudia kuzaliwa, Hussein, mtoto mwingine katika nyumba ya Bibi Fatimatuz Zahra SA binti mpenzi wa Bwana Mtume Muhammad SAW.

 • Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Malaria

  Apr 23, 2017 11:22

  Tarehe 25 ya Jumanne ya wiki hii dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Malaria ambayo ilitangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Siku hiyo ilikuwa fursa kwa walimwengu kutambua vyema zaidi ugonjwa huo na nchi mbalimbali kujifunza kutokana na tajiriba na uzoefu wa nchi mbalimbali juu ya namna ya kudhibiti ugonjwa huo unaoua mamilioni ya watu.