Jan 11, 2018 08:50 UTC
  • Aplikeshni ya iGap
    Aplikeshni ya iGap

Makala yetu ya leo ya matukio ya sayansi na teknolojia nchini Iran na maeneo mengine duniani kati ya mengine ina habari kuhusu zawadi ya $250,000 kwa yeyote atayakedukua (hack) aplikesheni ya iGap.

Ukarabati wa mifupa Iran

Hivi karibuni watafiti wa vyuo vikuu vya  Tehran na Amir Kabir wamefanikiwa kuunda chombo maalumu chenye mada ya kukarabati mifupa iliyovunjika au kuharibika.

Kwa mujibu wa watafiti wa mradi huu, moja ya faida za mbinu waliyobuni ni kuwa hakutakuwa na haja tena ya kufanya upasuaji na pia muda wa matibabu utapungua kwani mgonjwa atapona haraka. Moja ya malengo muhimu ya uhandisi wa tishu za mwili ni kutenganisha seli na kuzikuza katika chombo maalumu chenye muundo wa 3D katika mazingira yaliyodhibitiwa na hatimaye kiungo kinachoundwa hupelekwa katika sehemu maalumu inayohitajika mwilini. Chombo ambacho huwekwa katika mwili wakati wa kukarabati baada ya kufikisha tishu katika eneo lililokusudiwa huharibika chenyewe.

Upandikizaji mifupa hutumika sana kwa ajili ya kuboresha na kukarabati mifupa iliyoharibika. Lakini ukarabati wa nuksani katika mifupa kwa kutumia uhandisi wa tishu ni njia bora zaidi isiyo na madhara kwani mbinu hii huenda sambamba na muundo wa mwili wa mgonja na ukarabati huo hukamilika baada ya muda pasina kuhisika kuwepo kiungo bandia kama vile chuma na kadhalika.

Matibabu yaliyopo hivi sasa ya ukarabati wa mifupa yana vizingiti kutokana na kutumiwa mbinu za Allograft na Autograft. Mbinu inayotumiwa zaidi hivi sasa ni Autograft katika kupandikiza mifupa. Mbinu hii hii hutumika katika kuunda mifupa ambapo mfupa huondolewa kutoka katika mwili wa mtu mmoja hadi mwingine. Mbinu hii hupelekea kuibuka matatizo mengi hasa katika mwili wa mtu ambaye anatolewa mfupa kupelekwa katika mwili wa mtu mwingine. Aidha kuna uwezekano mkubwa wa uvujaji wa damu na kuenea sumu katika mwili sambamba na kuhisika uchungu mkubwa. 

Wanasayasni Wairani wavumbua mbinu mpya ya kutibua mifupa

Chombo cha otomatiki cha kuratibu oxigeni

Katika mafanikio mengine ya kisayansi, watafiti wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Ukarabati au Rehabilitation Sciences nchini Iran wamefanikiwa kuunda chombo ambacho kinaratibu kwa njia ya otomatiki mashine ya oxigeni, inayojulikana kama  Oxygen Flow Meter,  inayotumiwa na wenye matatizo ya kupumua.  Chombo hicho kimeundwa kidijitali ili kiweze kufanya kazi kwa njia ya otomatiki na kuwasaidia watumizi ambao huwa na matatizo ya kupumua. Kwa msingi huo chombo hicho kinafanya kazi kwa mujibu wa mahitaji ya kupumua ya mgonjwa ambaye anakitumia. Kwa mfano iwapo muuguzi hayupo karibu, chombo hicho kinaweza kufikisha oxigeni inayohitajika kwa mgonjwa kwa njia ya otomatiki. Kwa kawaida chombo  cha oxygeni hufanya kazi kwa kutegemea usimamizi wa mtu anayekitumia au muuguzi na hivyo oxigeni huongezwa au kupunguzwa kutokana na maamuzi yanayochukuliwa. Baadhi ya wakati yamkini mgonjwa akapokea oxigeni kupita kiasi na hali hiyo kupelekea tatizo la kuibuka kile kinachotajwa kuwa ni sumu ya oxigeni au oxygen intoxication. Aidha wakati mwingine yamkini mgonjwa akawa hawezi kupokea oxigeni ya kutosha na hivyo kuhatarisha maisha yake. Ni kwa msingi huo ndio kukawa na udharura wa kuibua mfumo wa otomatiki katika chambo cha Oxygen Flow Meter ili oxigeni iweze kutumika kwa msingi wa mahitaji ya mgonjwa.

Chombo cha Oxigeni

Chombo hiki kinachojulikana kama  pulse oximeter pia kimeundwa katika maeneo mengine duniani, lakini  kile likochoundwa na wataalamu Wairani kina baadhi ya sifa za kipekee. Kimsingi chombo hiki cha pulse oximeter huunganishwa na kidole cha mkononi  na kutuma ripoti kuhusu hali ya kimwili katika ile mashine ya oxigeni inayojulikana kama oxygen flow meter ambayo hapo hupima kwa njia ya otomatiki oxigeni anayopaswa kuitumia mgonjwa. Mpigo wa moyo wa mgonjwa huweza kuonekana katika chombo hicho na pia kinaweza kuonyesha iwapo oxigeni imakatika na kuwaonya walio karibu na mgonjwa.

Utumizi wa kupindukia wa michezo ya kompyuta au michezo ya video kutambuliwa kama ugonjwa wa kiakili

Shirika la Afya Duniani WHO linatafakari kutambua utumizi kupita kiasi wa michezo ya video au kompyuta kuwa tatizo la kisaikolojia ambalo kwa Kiingereza linajulikana kama Gaming Disorder.

Katika miaka ya hivi karibuni wanasaikolojia wamekuwa wakijadili iwapo watambue utumizi wa kupindukia wa michezo ya video au kompyuta kuwa ni tatizo la kiakili au la. WHO inaonekana kukaribia kutambua utumizi kupita kiasi wa michezo ya video au kompyuta yaani 'gaming disorder' kuwa tatizo la kisaikolojia.

Kwa mujibu wa rasimu ya orodha ya mwaka 2018 ya magonjwa iliyotayarishwa na  WHO, utumizi wa kupindukia wa michezo ya video na kompyuta unatambuliwa kama aina moja ya uraibu. Wataalamu wanasema iwapo michezo hiyo ya kidijitali itapewa umuhimu na kipaumbele kuliko shughuli zingine za kawaida za kimaisha basi huo unaweza kutajwa kuwa ni uraibu unaohitajia matibabu.

Mchezo wa Kompyuta

Ni wazi kuwa uraibu wa michezo ya video au kompyuta miongoni mwa baadhi ya jamaa katika familia hivi sasa ni tatizo sugu sana. Kutumiwa michezo hiyo kwa muda mrefu na kwa njia isiyofaa ni chanzo cha kuvurugika mazingira ya familia na hutikisa misingi ya ndoa, kudhoofisha uhusiano wa kindoa na uhusiano wa watoto na wazazi.

Watu wenye uraibu wa intaneti au michezo ya kompyuta hutumia wakati wao wa mapumziko au hata kazi wakiwa katika shughuli za kikompyuta.

Kuna kina mama au baba ambao wakiwa nyumbani au kazini hutumbukia katika mitandao ya intaneti na kijamii au michezo ya kompyuta na video na huwa hawana wakati kwa ajili ya familia ua kazi zao. Hali hii ikiendelea husababisha matatizo na yamkini wengine wakapoteza ajira ua kupelekea familia kusambaratika.

Aidha watoto ambao ni waraibu wa michezo ya kompyuta au video ambayo siku hizi pia inatumia intaneti  hukosa hamu ya kuwa na uhusiano na wengine au uhusiano huo huwa mdogo sana, jambo ambalo huwa na athari mbaya katika uhusiano  binafsi na wa kijamii na pia huathiri vibaya masomo shuleni au chuoni.

Ni kwa msingi huo ndio Shirika la Agya Duniani WHO likatafakari kutambua utumizi wa kupindukia wa michezo ya video au kompyuta kuwa tatizo la kisaikolojia linalohitaji matibabu kama maradhi mengine ya kiakili.

Dukua aplikesheni ya iGap upate zawadi ya $230,000

Shirika mola la Iran lenye kumiliki aplikesheni ya ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano inayojulikana kama iGap inayotumika katika simu erevu za mkononi na kompyuta limetoa changamoto kwa mtu yeyote atakayeweza kuidukua aplikesheni hiyo atapata zawadi ya dola laki $230,000.

iGap

Mkurugenzi na muasisi wa iGap Rassoul Kazemi amenukuliwa na Shirika la Habari la Fars akisema ujumbe mfupi na mafaili katika iGap ambayo yanatumia mfumo wa encryption hayawezi kuoenekana na yeyote isipokuwa mwenye kuyatuma au kuyapokea.

Siku hizi aplikesheni nyingi za mawasiliano zinatumia mfumo wa end to end encryption, kwa maana kuwa ni anayetuma au anayepokea tu ndio wanaoweza kusoma ujumbe katika simu zao.

Kazzemi amesema zawadi hiyo itapewa mtu yeyote atakayeweza kudukua safu mbili (pasina kuzingatia safu ya SSL) katika mfumo maalumu wa encyryption wa iGap na kubadilisha kodi katika mfumo kuwa maandishi yanayosomeka kawaida.

Aplikesheni ya iGap ina huduma kama vile za ujumbe, picha, video, sauti n.k. Aidha aplikesheni hiyo ya Kiirani ina huduma isiyo na malipo ya mazungumzo ya sauti kwa mara ya kwanza nchini Iran.

 

 

Tags

Maoni