Mei 05, 2018 13:38 UTC
  • Mafanikio ya wanasayansi Wairani katika matibabu ya moyo

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika makala hii ambayo huangazia mafanikio ya sayansi na teknolojia nchini Iran na maeneo mengine duniani. Kuweni nasi hadi mwisho.

Hivi karibuni wanasayansi Wairani walivumbua mbinu mpya ya kukarabati tishu za misuli ya moyo  kwa kutumia mashine ya uchapishaji au printer ya muundo wa 3D. Moja ya matatizo makubwa katika kutibu moyo baada ya mshutuko wa moyo ni kiungo hicho kutokuwa na uwezo wa kurejea chenyewe katika hali yake ya kawaida. Ili kutatua tatzio hilo, watafiti wameweza kuchapisha picha wanzohitajia katika kukarabati kiungo hicho ambapo seluli za moyo zilizochapishwa kwa muundo wa 3D  hutumiwa katika kutubi myo wa mgonjwa. Vipande vidogo vidogo vya moyo vilivyochapishwa katika muundo wa 3D huwa na umuhimu mkubwa katika kutibu moyo uliopoteza seli zake baada ya mshtuko. Ni wanasayansi wachache duniani ambao wameweza kupata mafanikio sawa na hayo ya watafiti Wairani.

Hivi karibuni, watafiti Wairani walipata mafanikio mapya katika sekta ya teknolojia ya nano. Wanasayansi Wairani wamefanikiwa kuunda spray yenye uwezo wa kuangamiza virusi au vijidudu katika vidonda. Aidha Wanasayansi Wairani wameweza kuzalisha uzi wenye mada za kioo ambao una uwezo wa kustahamili moto. Halikadhalika Wanasayansi Wairani wamefanikiwa kutumia teknolojia ya nano kubuni mbinu ya kufunga bidhaa ambayo kinyume cha plasitiki, si haribifu kwa mazingira. Hebu sasa tuangazia mafanikio hayo.

Kama ulivuosikia hapo, wanasayansi Wairani wameunda spray yenye uwezo wa kuagamiza vijidudu na kuondoa uchafu katika vidonda kwa kutumia teknolojia ya nano. Spray hii ina uwezo mkubwa wa kuaganmiza vijidudu  vyenye kusababisha magonjwa katika muda mfupi wa dakika tano. Nukta za kipekee za spray hii ya vidonda ni kuwa haiumizi mwili, haina harufu, haina alkoli, haina rangi, na huharakisha kupona kidonda.

Kwingineko, watafiti wa Kitivo cha Sekta ya Nguo katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Amir Kabir mjini Tehran, wamefanikiwa kutumia teknolojia ya nano kuzalisha uzi wenye mada za kioo ambao unaweza kustahamili miale ya moto. Kwa hivyo uzi huo unaweza kutumika kuzalisha mavazi maalumu yaisiyochomeka. Wahusika katika mradi huu wanasema vitambaa hivyo vinaweza kutegeneza nguo za kutumika katika sekta ambazo zinahitaji mavazi yenye kustahamili moto au joto kali n.k.

Katika sekta ya kufunga au kupakia bidhaa, wanasayansi Wairani, katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Kilimo na Mali Asili cha mji wa Sari kaskazini mwa Iran na Chuo Kikuu cha Tabriz kaskazini magharibi mwa Iran, wamefanikiwa kutumia teknolojia ya nano kubuni mbinu  ya kufunga bidhaa ambayo kinyume cha mada za plastiki, si hatari kwa mazingira. Hivi sasa kote dunaini, idadi kubwa ya mada zainazotumiwa kufunga bidhaa za chakula huwa zimeundwa kwa mada haribifu kwa mazingira kama vile plasitiki, chupa , metali. Mada hizo zikitupwa kama taka hurundikana kwa muda wa miaka mingi  na hivyo kupelekea kuharibika mazingira.

Ni kwa msingi huu ndio kukawa kunafanyika utafiti kwa lengo la kubuni mbinu mbadala ya kupakia chakula ambayo inatumia mada zisizokuwa haribifu kwa mazingira na ambazo huharibika haraka zikutupwa. Watafiti Wairani pia nao wako mbioni kubuni mbinu ambazo zitaokoa mazingira ya dunia. Katika mradi hu wa watafiti Wairani wanatumia mada zenye proteini, wanga na lipidi kubuni mbinu za kufunga bidhaa za vyakula. Pakiti hizo za kufunga bidhaa za chakula zilizoundwa na watafiti Wairani huwa na uwezo wa kuharibika haraka zinapotupwa. Hatahivyo nukta hasi katika mbinu hii ni kuwa iwapo chombo cha kupakia bidhaa  kitawekwa karibu na moto, joto au mahala penye unyevu basi chakula kilichofungiwa bidhaa hiyo kitaharibika haraka. Kwa msingi huo utumizi wa mbinu hiyo bado si mkubwa na wanasayansi wangali wanatafakari kuhusu njia za kuiboresha.

Wakulima wa ngano barani Afrika wana sababu ya kutabasamu kutokana na mradi wa utafiti na ustawi ambao unaboresha zao lao.

Wakulima wa ngano katika nchi kadhaa za Afrika, ambazo ni Benin, Kodivaa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Ethiopia, Ghana, Kenya, Lesotho, Madagascar, Mali, Mauritania, Niger, Nigeria, Senegal, Sierra Leone, Sudan, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe, wananufaika na mradi wenye lengo la kuongeza zao lao na hivyo kuhakikisha ngano inaweza kukidhi mahitaji ya jamii.

Kama tunavyojua, ngano ni chanzo muhimu cha vitamin, madini na wanga, nyuzi au fiber, aside ya foliki, antioxidanti n.k. Virutubisho hivi ni muhimu na huweza kupunguza au kukabiliana na magonjwa mengi ambayo yanawakumba watu wa bara Afrika. Pamoja na umuhimu huo wa ngano, zao hilo bado halikuzwi vya kutosha barani Afrika na kuna changamoto nyingi kama vile mbegu duni, wadudu waharibifu kwa mimea na magonjwa pamoja na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame wa muda mrefu na mafuriko.

Hivi sasa bara la Afrika hutegemea sana ngano iliyoagizwa kutoka nje ya bara hilo na hivyo kutoa pigo kwa pato ndogo la fedha za kigeni  katika nchi za bara hilo. Kwa mfano, asilimia 80 ya ngano ya Kenya hulimwa na wakulima wadogo na huweza kukidhi asilimia 20 tu ya hitajio la nchi hiyo.

Lakini sasa kwa msaada wa mradi wa Uungaji Mkono wa Utafiti wa Kilimo kwa Ajili ya Ustawi wa Mazao wa Kistratijia Afrika (SARD-SC), wanasayansi kutoka nchi 12 za Afrika hivi sasa wanabadilishana maarifa na uzoefu kuhusu kupunguza changamoto zitokanazo na uzalishaji ngano kwa kutumia teknolojia mpya sambamba na kuzalisha mbegu mpya.

 

Na wiki iliyopita Iran ilikuwa mwenyeji wa mashindano ya 13 ya kimataifa ya roboti maarufu kama RoboCup Iran Open competitions.   Mashindano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Maonyesho hapa mjini Tehran kutoka Aprili 3-7.

Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo yalifunguliwa rasmi na Dr. Ali Akbar Velayati Mkuu mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Azad Islami.

Timu ya Chuo Kikuu Huria cha Azad Islami cha Qazvin iliibuka mshindi katika kitengo vha magari ya roboti yenye kufanya shughuli za uokozi. Nayo timu cha Chuo Kikuu cha Erangen-Nuremberg cha Ujerumani ilishika nafasi ya kwanza katika kitengo cha mashindnao ya soka ya roboti  huku Timu ya Chuo Kikuu cha Zheijiang cha China ikishika nafasi ya pili.

Kwa ujumla kulikuwa na timu 478 zilizoshindana katika katekogria 38 za mashindano ambapo kulikuwa na timu 11 za kigeni zikiwemo Uturuki, China, Ujerumani, Uingereza, Marekani, Singapore na India.

Awamu hii ya  mashindano ya 13 ya kimataifa ya roboti maarufu kama RoboCup Iran ilikuwa na kategoria sita muhimu ambazo zilikuwa ni RoboCupSoccer, RoboCupUokozi, RoboCup@Nyumbani, RoboCup@Kazini, RoboCup Vijana na IranOpenDeminer.

RoboCup ni mashindano ya kimataifa ambayo hufanyika maeneo mbali mbali ya dunia kwa lengo la utafiti ili kuimarisha sekta ya roboti erevu na kuboresha elimu kuhusu teknolojia mbali mbali.

 

 

Tags

Maoni