Feb 11, 2016 18:23 UTC

Wakati siku mia moja za rais mpya wa Tanzania DK, John Pombe Magufuli madarakani zikitimia,Watanzania wamemtaka rais huyo kuongeza kasi ya kuwabana mafisadi wanaohujumu uchumi wa nchi hiyo bila kuwaonea huruma.

Aidha raia wa nchi hiyo, wamemtaka Rais Magufuli kukuza uchumi sanjari na kutekeleza ahadi alizozitoa katika kampeni za uchaguzi uliopia, ambapo wamesema kuwa mengi ya aliyoyaahidi bado hajayatekeleza, ingawa amejitahidi kwa kiasi fulani.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam Omar Manji kwa taarifa kamili….

Bonyeza katika picha hapo juu kupata sauti.


Tags