Oct 31, 2016 15:13 UTC
  • Rais Magufuli: Kenya, mshirika nambari moja wa Tanzania kibiashara barani Afrika

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amekanusha madai kuwa serikali yake inazipuuza nchi jirani na kujikita zaidi katika masuala ya ndani.

Akizungumza Jumatatu akiwa katika safari yake ya kwanza nchini Kenya tangu aingie madarakani Novemba mwaka jana , Dkt. Magufuli amesema daima amekuwa akiwasiliana na Rais Uhuru Kenyatta kwa njia ya simu. Ameongeza kuwa Tanzania inaitambua Kenya kama 'mshirika wetu nambari moja wa kibiashara barani Afrika.' Amesema safari yake nchini Kenya inalenga kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi mbili ambao umekuwa mzuri tokea siku za nyuma. Magufuli amesema amemfahamisha Rais Kenyatta kuhusu uhalisia wa mambo nchini Tanzania ambao ni kuwashurutisha Watanzanai walipe kodi na kupambana na ufisaid ili nchi isonge mbele.

Rais Magufuli (kushoto) na Rais Kenyatta

Rais Magufuli amekaribishwa kwa taadhima na heshima kubwa iliyojumuisha kukagua gwaride kamili la jeshi iliyoandamana na mizinga 21. Punde baada ya kuwasili, Rais Maguduli aliweka shada la maua katika kaburi la mwanzilishi wa taifa la Kenya, Mzee Jomo Kenyatta kabla ya kuelekea Ikulu ya Rais kwa mapokezi rasmi na mazungumzo na mwenyeji wake. Viongozi hao wamejadili masuala ya uhusiano wa nchi mbili na kieneo.

 

Tags