Apr 15, 2018 08:00 UTC
  •  Fatma Karume ashinda Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika

Mwanasheria wa kujitegemea nchini Tanzania Fatma Karume ameshinda nafasi ya urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Lawyers Society – TLS) nchini Tanzania kufuatia uchaguzi uliofanyika jana mkoani Arusha.

Binti huyo wa Rais mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume ameshinda kiti hicho cha urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika na kumrithiTanganyika  akichukua nafasi ya aliyekuwa Rais wa chama hicho, Tundu Lissu ambaye muda wake umemalizika.

Fatma Karume ameshinda kiti hicho kwa kura 820 akimuacha mbali mpinzani wake wakili Godwin Ngwilimi aliyepata kura 363.

Katika uchaguzi huo, Dkt. Rugemeleza Nshala amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa chama hicho. Aidha, Ndugu Omar Shaaban amechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar Lawyers Society.

Kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho, Uongozi wa TLS hudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, na baada ya hapo viongozi wengine huchaguliwa.

Zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa  Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, (TLS) 

Katika uchaguzi huo uliofanyika mkoani Arusha, kaskazini mwa Tanzania, Kamati ya Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, (TLS) iliyoundwa kujadili uamuzi wa Mwanasheria wa Mkuu wa Serikali (AG) wa kuzifanyia mabadiliko kanuni za uchaguzi wa chama hicho imesema,mwanasheria mkuu huyo hakuwa na mamlaka ya kufanya mabadiliko yoyote.

Makamu wa Rais wa TLS ambaye amemaliza muda wake, Godwin Ngwilimi, ametoa hoja hiyo na kumtaka mjumbe wa Baraza la uongozi, Jeremiah Mtobesya kusoma mapendekezo hayo ambayo yalisema Mwanasheria Mkuu wa serikali hakuwa na Mamlaka ya kufanya mabadiliko bali kuyachapisha kwenye gazeti la serikali.

Maoni