Jan 19, 2019 03:01 UTC
  • Kiongozi wa kundi la kigaidi la al Qaida Libya aangamizwa

Ripoiti kutoka Libya zinasema kuwa kinara wa kundi la kigaidi la al Qaida nchini humo ameuawa katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.

Vyombo vya jeshi la Libya limetangaza kuwa, Abdul Munim Salim Khalfa al Hasnawi maarufu kwa jila la Abu Talha Al-Libi aliuawa mapema jana Ijumaa katika operesheni ya Jeshi la Taifa iliyofanyika katika eneo la Al-Qarda Al-Shati karibu na mji wa Sabha huko kusini mwa Libya.

Ripoti zinasema kuwa, askari wa Libya walishambulia nyumba ya Abu Talha Al-Libi na kumuua yeye na wenzake kadhaa. Ripoti hiyo inasema kuwa Jeshi la Taifa la Libya linaendelea na operesheni yake katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo. 

Abu Talha Al-Libi ni miongoni mwa vinara mashuhuri wa kundi la kigaidi la al Qaida na mmoja kati ya waasisi wa kundi la kigaidi la Jabhatu Nusra nchini Syria. 

Libya ilitumbukia katika machafuko ya ndani mwaka 2011 baada ya majeshi ya Marekani na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kuivamia nchi hiyo na kuondolewa madarakani Muammar Gaddafi. Tangu wakati huo baadhi ya maeneo ya Libya yamekuwa wakidhibitiwa na makundi la kigaidi kama ya al Qaida na Daesh.    

Tags